Friday, July 4, 2025
spot_img

YANGA YATAJWA KUSAJILI WAKALI WATANO

Beki wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Bakari Malima, ‘Jembe Ulaya’, amesema klabu yake inatakiwa kusajili wachezaji wapya watano kwa ajili ya msimu ijayo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingine.

Tayari dirisha kubwa la usajili la wachezaji wapya limefunguliwa Julai mosi, mwaka huu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Malima alisema na pamoja kikosi cha Yanga kuonekana ni kizuri, lakini kuna umuhimu wa kuongeza wachezaji wapya ili waendelee kutwaa mataji.

Malima ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu ya vijana Yanga, alisema uongozi wa klabu hiyo, unatakiwa kufanya usajili wa maana katika idara ya mabeki, kiungo mkabaji wa chini, washambuliaji na winga.

Beki huyo alisema anahitaji kuona anasajiliwa beki mmoja wa kati, kiungo mmoja, washambuliaji wawili na winga mmoja ili kukiongezea anguvu kikosi hicho

Nyota huyo wa zamani alisema kwa sasa Yanga hawana winga asilia mwenye uwezo wa kucheza kama alivyokuwa Mrisho Ngasa na Simon Msuva.

Malima alisema pamoja na Yanga wanaonekana wanakombinesheni nzuri kutokana na wachezaji wao wamekaa kwa misimu mitatu mfululizo, baadhi ya nyota wao wanachezea uzoefu, kwani umri umewatupa mkono na kunahitajika nafasi zao kuongezewa nguvu mpya ili waendelee kuwa katika ubora wao.

Alisema kwa kuwa Yanga wanajiandaa na msimu mpya, wanahitaji kufanya usajili kwa malengo kama wanahitaji kufanya vizuri na baadaye kubeba mataji.

Yanga ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara nne mfululizo, msimu uliopita waliishia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya