Sunday, May 11, 2025
spot_img

MSIMU WA MAUZO YA UFUTA KIDIJITALI WAFUNGULIWA

ZERUBABEL CHUMA

MSIMU wa mauzo ya zao la ufuta kwa mfumo wa kidijitali umefunguliwa kuanzia April 25, 2025.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo na Mamlaka ya Udhibiti wa Mazao Mchanganyiko (COPRA), imeeleza kuwa utaratibu kwa wauzaji na wanunuzi wa zao hilo kwa msimu huu wa mauzo, utakuwa wa mfumo wa stakabadhi za ghala kwa kutumia minada ya kidijitali katika mikoa yote inayozalisha zao hilo.

Taarifa hiyo inawataka wananchi, wanunuzi na wadau wa kilimo kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali Januari 9, mwaka huu kuhusu orodha ya mazao ya kunde na mbegu za mafuta kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi za ghala na minada ya kidijitali kwa msimu wa 2024/2025.  

COPRA inawaonya wafanyabiashara wa mazao hayo kuwa hawaruhusiwi kununua mazao yaliyotajwa kupitia tangazo la serikali nje ya mfumo wa stakabadhi za ghala na kwamba ratiba za minada zitatolewa na COPRA yenyewe.

Aidha, COPRA inawarai wafanyabiashara kutojihusisha na ununuzi nje ya mfumo rasmi au kusafirisha mazao nje ya nchi bila vibali halali na au kughushi vibali kwani atakayegundulika kufanya vitendo hivyo atakuwa amekiuka sheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Inazitaja hatua zitakazochukuliwa kuwa ni pamoja na kutaifisha mazao yatayogundulika kununuliwa au kusafirishwa kinyume na utaratibu, kuzuiwa kushiriki katika shughuli za ununuzi wa mazao ndani ya nchi, kutozwa faini pamoja na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa kifungu cha 22 cha sheria ya usalama wa chakula, sura ya 249.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya