Saturday, April 19, 2025
spot_img

UJENZI DARAJA LA JANGWANI MBIONI KUANZA

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewatoa hofu wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusiana na hali ya usalama katika mkoa huo huku akisisitiza kwamba hakuna mtu atakaeweza kuvuruga amani ndani ya mkoa huo huku akitoa wito kwa yeyote mwenye malalamiko kuhusu jambo lolote kufika kwenye vyombo husika ili lifanyiwe kazi.

Ameyasema hayo leo Aprili 18, ikiwa ni katika kusisitiza taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa jana kuhusu taarifa zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii za kuhimiza wananchi kujitokeza kushiriki maandamano yanayoelezwa kuwa ni ya “kuishinikiza serikali” kumuachia huru Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambaye anashikiliwa na vyombo vya dola.

Mapema jana, Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro, lilitoa woto kwa wananchi kutoshiriki tukio hilo ambalo linaweza kutishia usalama wa Jiji la Dar es Salaam, na kwamba suala hilo linapaswa kuachwa liendelee kufanyiwa kazi na Mahakama ambayo kisheria haipaswi kuingiliwa na vyombo vingine vya kimamlaka.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi mbali mbali ya miundo mbinu ndani ya mkoa huo hasa katika miradi ya barabara, madaraja na vivuko kutokana na fedha zinazopatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwa ni pamoja na wadau wa maendeleo kama vile Benki ya Dunia (WB) na benki ya maendeleo africa (AFDB)

Aidha mkuu wa mkoa ametoa taarifa kwa wakazi wa Dar es salaam kuhusu ujenzi wa daraja la jangwani amesema kuwa hatua ya kwanza ya mkandarasi kusaini mkataba imeshapita na sasa mkandarasi anajiandaa kuingia saiti ambapo ameanza kwa kujenga makazi ya kuhifadhia vifaa katika kipindi chote cha ujenzi wa daraja hilo wakati huo akisubiri kulipwa malipo ya awali ili aweze kuanza ujenzi akisisitiza kwamba ni nia ya serikali ya awamu ya sita kukamilisha mradi huo.

Katika hatua nyingine Chalamila amesema kuwa serikali inaendelea na juhudi za kuimarisha huduma za usadiri wa mwendokasi katika Jiji la Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kuendelea kukamilisha ujenzi wa awamu ya nne ni mradi wa barabara yenye urefu wa kilomita 30.

Amesema serikali kupitia wizara ya TAMISEMI inaendelea na mchakato wa kutafuta wadau watakaoshirikiana na serikali katika kufanikisha upatikanaji wa mabasi kwenye njia zote ambazo zimeshakamilika, ili kuwarahisishia wakazi wa Dar es Salaam huduma za usafiri

Mkuu wa mkoa amewataka wananchi wa Dar es salaam kutumia kipindi hiki cha sikukuu ya pasaka kudumisha amani na utulivu lakini pia amewataka kumuombea Mhe. Mohamed Mchengerwa, ambaye ni Waziri wa TAMISEMI, anayetarajia kuwasilisha bajeti za wizara hiyo Bungeni mnamo Aprili 22 2025, bajeti ambayo inakadiriwa kuwa ya Trilioni 11, huku mkoa wa Dar es Salaam pekee ukiwa umeomba bajeti ya trilioni 1, ili kuboresha na kuimarisha huduma za kijamii ndani ya mkoa huo

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya