Saturday, April 19, 2025
spot_img

SANAA NI UCHUMI-MAJALIWA

ZERUBABEL CHUMA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema serikali imejidhatiti kuendelea kukuza na kuimarisha sanaa nchini ikiwa ni moja ya sekta rasmi ya kiuchumi.

Majaliwa alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa akihutubia Kongamano la Chama cha Wafawidhi wa Matukio Tanzania, linalofanyika Olasiti Garden, Mkoani Arusha.

Alisema fani ya ushereheshaji ni Uchumi na serikali kwa kutambua hilo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliridhia kaunzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa unaokopesha hadi Shilingi milioni 100 kwa wasanii, wakiwemo washereheshaji ili waweze kujiimarisha kimitaji na vitendea kazi.

“Kupitia maboresho ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999, yaliyofanyika mwaka 2022, serikali imeanzisha tozo ya hakimiliki (copyright levy) ambapo asilimia 60 ya makusanyo inakuja kwenu moja kwa moja na asilimia nyingine 10 inakuja kwenu kupitia mfuko,” alisema.

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa alihutubia kongomano la Chama cha Wafawidhi wa Matukio Tanzania, hivi karibuini.

Aidha, Majaliwa alisema serikali inatarajia kujenga ukumbi wa kimataifa ya sanaa na michezo ‘Arts and Sports Arena,’ utakaogharimu Shilingi bilioni 300.

“Haya yote ni maono ya Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alisema Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa, aliaigiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kushirikiana na Chama cha Kisima cha Mafanikio kuandaa miongozo, mafunzo ya kitaaluma na mfumo wa urasimishaji wa washereheshaji nchini.

“Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), endeleeni kushirikiana na Kisima cha Mafanikio kukuza matumizi sahihi ya Lugha ya Kiswahili kwenye majukwaa mbalimbali,” alisema.

Kwa Upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi alimshukuru Rais Dkt. Samia kwa uongozi mahiri na kwa kutoa fursa kwa watanzania kukuza vipaji vyao na kuendeleza stadi za kazi na taaluma katika tasnia mbalimbali ikiwemo ya ushereheshaji na upangaji wa matukio.

“Hakika Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kulea vipaji na kuvipa nafasi kuonekana pamoja na kutenda kazi zao kama ilivyo kwenu watu wa Kisima cha Mafanikio,” aliserma Kabudi.

Mwenyekiti wa chama hicho, Ester Kimweri aliipongeza serikali kwa kusimamia uzalendo.

“Sisi wadau wa sekta hii tunapenda kuonesha nia yetu ya dhati kuendelea kuunga mkono juhudi hizi kwa vitendo kwa kuelimisha, kuhamasisha, kuburudisha na kufundisha na tutaendelea kuheshimu sheria, kulinda rasilimali, mali za umma na kushiriki shughuli za maendeleo ya jamii,” alisema kimweri.

MATUKIO KATIKA PICHA WAZIRI MKUU AKIHUTUBIA KONGAMANO LA WAFAWIDHI WA MATUKIO.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya