Saturday, April 19, 2025
spot_img

MABALOZI KUTALII SERENGETI, NGORONGORO NA ZANZIBAR

RIPOTA PANORAMA

MABALOZI wa mataifa mbalimbali waliopo hapa nchini wanafanya ziara ya kitalii katika Mbunga ya Wanyana ya Serengeti, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoto na maeneo ya kitalii yaliyopo Zanzibar.

Ziara hiyo ya kitalii kwa mabalozi imeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ziara ya kitalii kwa mabalozi, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko aliipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuandaa ziara hiyo.

Dkt. Biteko alisema katika ziara hiyo, mabalozi wa mataifa mbalimbali waliopo Tanzania watapata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Zanzibar na Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

“Tanzania ni sehemu nzuri ya utalii duniani na ni imani yangu kuwa mtapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ukiwemo Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio kikubwa duniani.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko akisalimiana na mabalozi waliofika kwenye uzinduzi wa ziara ya kitalii kwa mabalozi wa mataifa mbalimbali waliopo Tanzania.

“Mtatembelea pia Mji Mkongwe, Zanzibar na pia mtaweza kujifunza maneno machache ya Lugha ya Kiswahili kupitia ziara hii. Tuna maziwa na mito mingi na maeneo mengine ya kihistoria kama Bagamoyo na vijiji vya wamasai,” alisema Dkt. Biteko.

Alitoa rai kwa mabalozi kuendelea kukuza ushirikiano kati na mataifa yao na Tanzania na kwamba watakuwa mabalozi wazuri wa utalii wa Tanzania.

Waziri wa Maliasili na Utalii. Balozi Pindi Chana.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana alisema ujumbe huo wa mabalozi utatembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Ngorongoro, Serengeti na Mlima Kilimanjaro.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi alisema baada ya safari ya Arusha, Kilimanjaro na Zanzibar, mabalozi hao wataitangaza Tanzania kimataifa.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi.

Balozi wa Comoro nchini na kiongozi wa mabalozi waliopo Tanzania, Ahmada El Badaoui Mohammed Fakhi alisema kwa takribani miaka 11 aliyokuwepo nchini, hii ni mara yake ya kwanza kufanya ziara ya aina hiyo.

“Kwa niaba ya waheshimiwa mabalozi wote, niipongeze Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashriki na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuandaa tukio hili,” alisema.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya