Saturday, April 19, 2025
spot_img

BUNGE MARATHON KUJENGA BUNGE SEKONDARI WAVULANA

ZERUBABEL CHUMA,

Dar es Salaam

FEDHA zilizokusanywa katika mbio za hisani za Bunge zitatumika kujenga Shule ya Sekondari ya Bunge Wavulana.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa akizindua mbio hizo zilizowashirikisha wabunge, watumishi wa Bunge na wadau wengine wa ndani ya nje ya nchi.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema fedha zilizokusanywa zitatumika kama zilivyokusudiwa kujenga Shule ya Sekondari ya Bunge Wavulana itakayokuwa na uwezo wa kusajili wanafunzi kati ya 300 hadi 350.

Alisema shule hiyo itakuwa na kidato cha tano na sita na itajengwa katika eneo la Kikombo, jijini Dodoma, karibu kidogo na shule ya wasichana iliyojengwa na wabunge wanawake mwaka 2020.

“Ninawapongeza sana wabunge wenzangu kwa kuweka alama na kugusa maisha ya Watanzania na watoto wetu wa kiume watakaopata fursa ya kusoma katika shule hiyo,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema ujenzi wa shule hiyo ni mpango wa Bunge wa kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia suluhu Hassan kukuza na kuendeleza sekta ya elimu.

Majaliwa amesema shule hiyo itakuwa ya bweni yenye maabara nne za biolojia, kemia, fizikia na jiografia, maktaba, bwalo la chakula, nyumba za walimu pamoja na viwanja vya michezo.

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson aliyeshiriki mbio hizo, amewashukuru washiriki wote kwa kuwaunga mkono wabunge na kueleza kuwa Bunge limeonesha mfano wa kujali watoto wote.

Awali, mwenyekiti wa mbio za hisani za Bunge, Festo Sanga alisema lengo la mbio hizo ni kukusanya fedha za ujenzi wa shule ya wavulana. Mbio hizo zilihusisha watu zaidi ya 4,000.

MATUKIO KATIKA PICHA MBIO ZA HISANI ZA BUNGE.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya