RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana, April 8, 2025 alitembelea Makumbusho ya Rais wa kwanza na muasisi wa Taifa la Angola, Hayati António Agostinho Neto, katika eneo la Public Square, jijini Luanda, Angola.
Rais Dkt. Samia alipokelewa kwa heshima ya kijeshi katika eneo hilo la makumbusho na kisha kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa Rais Neto.

Picha ya Hayati António Agostinho Neto, Rais wa Kwanza wa Angola.






