Thursday, July 17, 2025
spot_img

MIRADI YA UTALII KULETA MAGEUZI

RIPOTA PANORAMA – SINGIDA

Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kuimarisha Sekta ya Utalii kwa kuweka mikakati mbalimbali ya kuchechemua ongezeko la watalii na kukuza pato la Taifa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Utalii (TDL).

Akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao kazi cha viongozi wa taasisi za wizara hiyo zinazotekeleza miradi kupitia  mfuko huo, mkoani Singida, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Maliasili na Utalii, Abdullah Mvungi amesema kikao hicho kimelenga kupata uelewa wa pamoja wa uboreshaji wa mipango na mikakati ya utekelezaji wa miradi hiyo ya kimkakati inayolenga kutoa matokeo chanya kwa jamii.

Mvungi amesema serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa vitendo  kukuza utalii kupitia mfuko huo hivyo ni vyema kwa viongozi wa taasisi zinazotekeleza miradi kupitia mfuko huo kusimamia kikamilifu miradi itakayotekelezwa kwa maslahi mapana ya Taifa.

Aidha, Mvungi amesema utekelezaji wa miradi hiyo umelenga kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje, kuongeza mapato ya fedha za ndani na za kigeni, kuongeza ajira pamoja na kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia Sekta ya Utalii.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii, John Mapepele ameeleza kuwa wizara itaendelea kutoa taarifa kwa umma  kuhusu maendeleo ya mafanikio yanayopatikana katika  miradi.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya