UKITAKA kuliona au kusali ndani ya Kanisa Katoliki la kihistoria lenye miaka zaidi ya 145 tangu lilipojengwa, nenda katalii kwenye makumbusho ya Dkt. David Livingstone, iliyopo Manispaa ya Ujiji – Kigoma, Mkoa wa Kigoma.
Kanisa hilo la kihistoria lililojengwa mwaka 1879 na wakoloni wa kijerumani; hadi sasa linatumiwa na waumini wengi wa dini ya kikristu kutoka ulimwengu kote kuabudu huku watalii wengi kutoka Ulaya na Marekani wakienda hapo kutalii na kupiga picha.
Ni moja ya majengo yaliyosanifiwa na mabingwa wa usanifu majengo wa mwashoni mwa karne 18 na limejengwa kwa ustadi mkubwa, likiwa na nguzo imara ambazo hazina nondo.

Mariam Mkonya, Mhifadhi Mkuu wa Malikale, Makumbusho ya Dkt. David Livingstone, iliyopo Ujiji, Kigoma akiwa amesimama mbele ya Kanisa Katoliki lililojengwa mwaka 1879, akielezea historia ya kanisa hilo.
Mhifadhi Mkuu wa Malikale, Makumbusho ya Dkt. David Livingstone, Miriam Mkonya, anasema katika Bara la Afrika, majengo ya aina hiyo yaliyopo sasa ni machache sana na yamekuwa yakitumiwa na wataalamu wa usanifu majengo, hususan kutoka Ulaya na Marekani kujifunza utaalamu wa usanifu majengo waliokuwa nao wasanifu majengo wa karne ya 18 na 19.
Anasema wataalamu wa usanifu mejengo wa hapa nchini na Afrika Mashariki wanaweza kupata elimu ya ziada ya usanifu majengo kwa kulitembelea kanisa hilo.
Ndilo kanisa la kwanza kujengwa katika Mkoa wa Kigoma na Padre wa kwanza wa kanisa hilo alitoka Australia.

Kanisa Katoliki la kihistoria lililopo Ujiji, Kigoma lililojengwa mwaka 1879 linavyoonekana kwa ndani.
Tanzania ina hazina kubwa ya urithi wa utamaduni ambao kwa hakika Watanzania wanapaswa kuufikia na kujionea pamoja na vivutio vingine, chimbuko la ukatoliki katika Mkoa wa Kigoma.
Tunajivunia ukatoliki na tunawaombea mapadri wa kwanza waliokuja kueneza injili