Thursday, March 13, 2025
spot_img

HISTORIA INAYOISHI IPO MAKUMBUSHO YA CHIFU MKWAWA

HISTORIA ya zaidi ya miaka 130 ya Kabila la Wahehe, lililopo Mkoa wa Iringa bado inaishi.

Historia hiyo inaishi katika makumbusho ya Chifu Mtwa Mkwawa Mkwavinyika iliyopo Kitongoji cha Wanji, Kijiji cha Kalenga, Kata ya Kalenga mkoani Iringa

Makumbusho ya Chifu Mkwawa ipo kilometa 10 kutoka mzunguko wa Samora uliopo Iringa mjini ambapo watalii au mtu anayetaka kuijua historia hiyo anaweza kufika ikitokea Iringa Mjini kwa kutumia usafiri wa pikipiki, bajaji au gari.

Kwa watalii wanatoka nje ya nchi au mikoa mbalimbali, wanaweza kufika Iringa kwa usafiri wa ndege na wakishatua uwanja wa ndege wa Iringa wanaweza kutumia usafiri wa pikipiki, bajaji na gari kufika makumbusho ya Chifu Mkwawa.

Katika makumbusho hiyo ndipo palipohifadhiwa fuvu la kichwa cha Chifu Mkwawa ambalo Wajerumani wanaamini kuwa fuvu hilo la Chifu wa Kitanzanmia  lilihifadhi ubongo wenye akili za ziada katika medani za vita.

Makumbusho hiyo, mbali na kuhifadhi fuvu la kichwa cha Chifu Mkwawa, pia imehifadhi historia ya machifu waliofuata wa kabila la wahehe baada ya  Chifu Mkwawa mwenyewe ambaye alifuatiwa na Chifu Sapi Mkwawa, Chifu Adam Sapi Mkwawa, Chifu Abdul Mkwawa na chifu wa sasa Mtwa Adam Mkwawa wa pili.

Makumbusho ya Chifu Mkwawa ilianzishwa mwaka 1954 ikisimamiwa na Idara ya Malikale lakini ilipofika mwaka 1957 ilihamishiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo.

Mwaka 1962 hadi 1964 iliwekwa chini ya Wizara ya Utamaduni na Vijana na 1964 hadi 1967 ilikuwa chini ya Ofisi ya Rais.

Mwaka 1967 hadi 1968 ilikuwa chini ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Maendeleo Vijijini kisha mwaka 1968 hadi 1980 ikawa chini ya Wizara ya Elimu na mwaka 1980 hadi 1984 ikawa chini ya Wizara ya Habari ya Utamaduni.

Mwaka 1984 mpaka 1985 ilikuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na 1985 hadi 1988 ilikuwa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Utamaduni, Vijana na Michezo.

Mwaka 1988 hadi 1990 ilipelekwa kuwa chini ya Wizara ya Utumishi wa Umma na Ustawi wa Jamii na 1990 mpaka 1999 ikawa chini ya Wizara ya Elimu na Utamaduni.

Kuanzia 1999 hadi 2019 makumbusho hiyo iliwekwa chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii lakini ilipofika mwaka 2019 pamoja na kuwa chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Serikali iliamua kuiweka chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Uamuzi wa kuiweka Makumbusho ya Chifu Mkwawa chini ya TANAPA ulifikiwa baada ya kuwa haifanyi vizuri shughuli zake hivyo TANAPA ilipewa jukumu ya kuisimamia.  

Chifu Mtwa Mkwawa.

Chini ya TANAPA, miundombinu ya kufika kwenye makumbusho hiyo imeimarishwa na historia iliyohifadhiwa hapo inatunzwa kwa uangalifu mkubwa.

Aidha, kwa kutambua umuhimu wa kurithisha vizazi na vizazi historia ya makabila ya Tanzania, TANAPA imeweka viingilio vya chini kuingia na kutalii na au kujifunza historia ndani ya makumbusho hiyo.

Kwa watalii wa ndani ambao ni watu wazima, mtu  mmoja analipa Sh 2,360, watoto Sh 1,180. Watalii kutoka nje ya nchi, mtu mzima analipa Dola za Marekani 10 na kwa mtoto analipa Dola za Marekani 5. Wataalamu au wageni wenye vibali vya kuishi Tanzania wanalipa Dola za Marekani 5.  

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya