Tuesday, June 3, 2025
spot_img

VIUMBE HAI WENYE KASI ZAIDI DUNIANI

RIPOTA MAALUMU

REKODI ya viumbe hai wenye kasi zaidi duniani inashikiliwa na ndege, wakifuatiwa na samaki na mwisho ni viumbe hai watembeao ardhini  

Kwa mujibu Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) likinukuu ripoti mbalimbali za watafiti wa maisha na tabia za viumbe hai, sungura mwenye rangi ya hudhurungi anatajwa katika kundi la wanyama wa ardhini wenye kasi kubwa ya kukimbia duniani.

Sungura mwenye rangi ya hudhurungi

Sungura wa aina hii, wana miguu mirefu ya rangi nyeusi inayowawezesha kukimbia kwa kasi ya kilomita 77 kwa saa, kasi ambayo ni sawa na ile ya mbwa mwitu mwekundu.

Nyumbu mwenye rangi ya samawati naye anatajwa kwenye kundi la wanyama watembeao ardhini wenye kasi kubwa ya kukimbia duniani.

Nyumbu mwenye rangi ya samawati.

Pamoja naye, nyumbu mwenye rangi ya bluu, gazelle na springbok nao wanatajwa kuwa na kasi sawa naye ambayo ni kasi ya kilomita 80 kwa saa. Kasi ambayo inaikaribia ile ya Simba.

Samaki aina ya marlin, yeye kasi yake ya majini ni kilomita 80 kwa saa, lakini ripoti za hivi karibuni zinamtaja samaki aina ya sail kuwa na kasi zaidi zake.

Samaki aina ya marlin

Paa mwenye pembe ya kuchoma ambaye anafahamika pia kwa jina la swala pronghorn ni mnyama mwingine wa ardhini mwenye kasi zaidi ya kukimbia. Swala huyu ana uwezo wa kukimbia kilomita 98 kwa saa.

Swala pronghorn

Mbali ya samaki aina ya marlin na sail, rekodi zilizopo zinamtaja Samaki wa Tanga kuwa ndiye samaki mwenye kasi zaidi duniani akiwa na kasi ya kilomita 110 kwa saa akiwa ndani ya maji.

Samaki wa Tanga.

Duma anatajwa katika kundi la wanyama watembeao ardhini wenye kasi kubwa ya kukimbia duniani.

Duma.

Duma ana kasi kubwa mara tatu zaidi ya binadamu ambaye ana uwezo wa kukimbia kilomita takriban 36 kwa saa.

Bata bikini mwenye mabaya yenye ncha ni bata mkubwa zaidi duniani na ana uwezo wa kupaa kwa kasi ya kilomita 142 kwa saa.

Bata bikini.

Ndege msindikizaji ambaye ana mabawa marefu ana uwezo wa kukaa angani kwa zaidi ya wiki moja ana uwezo wa kupaa kwa kasi ya kilomita 153 kwa saa.

Ndege aina ya kipanga.

Ndege aina ya Spine Tailed Swift. Ni ndege mwenye rangi nyeupe shingoni na ana mkia uliochongoka. Ndege huyu ana uwezo wa kupaa kwa kasi ya kilomita 171 kwa saa.

Rekodi ya dunia ya kiumbe hai mwenye kasi zaidi inashikiliwa na ndege aina ya kipanga. Ndege huyu anapokuwa kwenye mawindo huruka juu umbali mrefu kisha hushuka kwa kasi ya zaidi ya kilomita 322 kwa saa.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya