MASHIRIKA YA HABARI
MAKAMU wa Rais wa Namibia, Netumbo Nandi Ndaitwah ametangazwa mshindi wa nafasi ya Rais nchini Namibia kwa kupata asilimia 57 ya kura zilizopigwa wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya kimataifa, Tume ya Uchaguzi ya Namibia imemtangaza Ndaitwah wa Chama cha South West African People’s Organisation (Swapo) kwa mshindi wa urais. akimbwaga mpinzni wake wa karibu, Panduleni Itula ayepata asilimia 26 ya kura zilizopigwa.
Ndaitwah anakuwa Rais wa kwanza mwanamke kuchaguliwa kuiongoza Naminia tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1990.
Hata hivyo, ushindi wake umepingwa na Itula ambaye tayari amekwishatangaza nia yake ya kukimbilia mahakamani kutokana na dosari zilizojitokeza wakati wa upigaji kura.
Vyombo vya habari nchini Namibia vimeripoti kuwa uchaguzi huo ulisusiwa na vyama vingi vya upinzani na wakati wa upigaji kura kulitokea tatizo la upungufu wa vifaa vya kupigia kura hivyo kulazimu kuongezwa siku tatu za kupiga kura.
Chama tawala cha Swapo ambacho Ndaitwah alikuwa mgombea wake kimekuwa madarakani nchini Namibia kwa miaka 34.