Monday, December 23, 2024
spot_img

KESI YA KIPANYA DHIDI YA MWIJAKU YAONDOLEWA

RIPOTA PANORAMA

MAHAKAMA Kuu, masijala ndogo ya Dar es Salaam, imeondoa kesi ya kashfa iliyofunguliwa na Ally Masoud Nyomwa, maarufu kwa jina la Masoud Kipanya dhidi ya Burton Mwemba Mwijaku kwa sababu ya dosari za usajili.

Kwa mujibu wa wakili wa Kipanya, Alloyce Komba kesi hiyo iliondolewa mahakamani na Jaji David Ngunyale, Oktoba 24, 2024 kabla hajatoa uamuzi wa mapingamizi manne ya kisheria ya mdaiwa Mwijaku yaliyokwisha sikilizwa kupitia kwa wakili wake, Gideon Opanda.

Kipanya aliwakilishwa mahakamani na mawakili wanne wakiongozwa na Wakili Alloyce Komba.

Jaji Ngunyale alisema Mahakama imebaini kuwa kesi iliyokuwa ikiendesha, ilisajiliwa kwa makosa kama kesi ya madai ya kawaida (normal civil suit) badala ya madai ya kashfa (defamation petition) kwa mujibu wa kanuni za sheria ya habari za mwaka 2019.

Alisema kutokana na dosari hiyo Mahakama inasitisha kuendelea na kesi ya msingi.

Kabla ya uamuzi huo, Jaji Ngunyale alitoa fursa kwa mawakili wa pande zote mbili kutoa maoni yao ya kisheria kuhusu dosari hiyo na nini kifanyike.

Wakili Komba ameieleza Tanzania PANORAMA kuwa baada ya kutolewa kwa fursa hiyo, aliiomba mahakama kuondoa kesi hiyo ili kumpa fursa nyingine mteja wake kufungua tena kesi kama ataamua kufanya hivyo.

Wakili Opanda aliomba kesi iondolewe kwa gharama kutokana usumbufu wa kushitakiwa mteja wake.

Mahakama ilitoa amri ya kuondoa kesi yenye dosari ya usajili bila gharama ya usumbufu kwa sababu hoja ya dosari ya usajili iliibuliwa na Mahakama yenyewe na sio na Wakili wa Mwijaku, hivyo hapaswi kunufaika nayo.

Katika kesi ya msingi, Kipanya alimshitaki Mwijaku kwa kumkashifu kupitia akaunti yake ya Instagram kwamba anafanya biashara haramu ya kuharibu vijana na kupitia katuni zake anahongwa ili kuwadhalilisha viongozi wa Serikali akiwemo Rais wa nchi.

Alidai mahakamani alipwe fidia ya Shilingi bil. 5.5 kwa madhara ya kashfa ya kushushiwa hadhi ambayo ameijenga katika jamii kwa zaidi ya miaka thelathini.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya