Thursday, June 5, 2025
spot_img

BUKOMBE WAPEWA MITUNGI YA GESI YA RUZUKU

MOHAMEDI SAIF

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) imetoa mitungi ya gesi kwe bei ya ruzuku kwa wakazi za Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.

Akizungumza wakati wa semina maalumu iliyoandaliwa na REA, Oktoba 10, 2024 kwa wakazi wa wilaya hiyo kabla ya kutoa mitungi ya ruzuku, Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage alisema wakati umefika wa kutumia nishati safi ya kupikia ili kuimarisha afya sambamba na kutunza mazingira.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan ni kinara wa ajenda ya nishati safi ya kupikia na anafanya kila analoweza ili wananchi wote wapate mishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu.

Akizungumza wakati wa Semina hiyo, Mhandisi Mwijage alisema Wakala umepewa jukumu la kuhakikisha bidhaa za Nishati Safi za Kupikia zinafika katika kila pembe ya nchi ili kumuwezesha kila mwananchi kuachana na matumizi ya Nishati isiyo safi na salama.

“Serikali kupitia REA imetoa ruzuku kwa bidhaa za nishati safi za kupikia ili kuhakikisha hakuna mwananchi anaachwa nyuma,” alisema.

Mhandisi Mwijage alisema kwa bidhaa za mitungi ya gesi (LPG), Serikali imeingia makubaliano na watoa huduma ya kusambaza mitungi 3,255 ya kilo sita kwa bei ya ruzuku kwenye kila wilaya.

“Kwa hapa Bukombe, mtoa huduma atakayesambaza mitungi ni Kampuni ya Manjis ambapo mitungi hii ya kilo sita ikiwa kamili na vichomeo vyake itatolewa kwa shilingi 17,500 tu ambayo ni sawa na nusu bei,” alisema Mhandisi Mwijage.

Wakazi wa Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita wakiwa katika foleni ya kununua mitungi ya gesi ya ruzuku hivi karibuni.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Paskasi Muragili ambaye aliwa mgeni rasmi kwenye semina hiyo alimshukuru Rais Samia kwa kutoa ruzuku katika bidhaa za nishati safi za kupikia.

“Leo ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa Bukombe, tunapokea mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku na hizi ni jitihada za Rais Samia na Serikali anayoiongoza,” alisema Muragili.

Alitoa rai kwa wananchi hao kujaza gesi kwenye mitungi hiyo kuhakikisha inapomalizika ili waendelea kutumia nishati safi ya kupikia.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, Yusuph Yusuph alisema REA inatekeleza dhamira ya Rais Samia kwa vitendo na iliyotolewa itaongeza uelewa wa matumizi ya nishati hiyo kwa wananchi.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya