Monday, December 23, 2024
spot_img

VITONGOJI 135 PWANI KUPATA UMEME

MOHAMED SAIF

VITONGOJI 135 vya Mkoa wa Pwani vipo mbioni kupata huduma ya umeme baada ya kupatikana kwa mkandarasi wa kutekeleza mradi wa usambazaji umeme kwenye vitongoji hivyo.

Mkandarasi atakayetekeleza mradi huo ni China Railway Construction Electrification Bureau Group Co. Ltd ya Uchina na alitambulishwa Septemba 25, 2024 na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge alisema kutekelezwa kwa mradi huo kutaufanya mkoa huo kuwa wa kimkakati kwa sababu nyenzo muhimu za kuchochea maendeleo kwa wananchi zinapatikana.

Kunenge aliipongeza REA kwa kutekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alitoa rai kwa mkandarasi kukamilisha kazi ndani ya muda ulio kwenye mkataba wake.

Alisema utaratibu wa kutambulisha wakandarasi ni mzuri kwa sababu unasaidia kutoa picha halisi ya hali ilivyokuwa kabla ya utekelezaji miradi na baada ya utekelezaji.

Mkurugenzi wa Umeme Vijijini wa REA Mkoa wa Pwani, Mhandisi Jones Olotu alisema mkoa huo una vijiji 417, kati ya hivyo 407 ambavyo ni sawa na asilimia 98 vimeunganishiwa umeme.

Alivitaja vijiji 10 ambavyo havijafikishiwa umeme kuwa vipo maeneo ya delta katika Wilaya ya Kibiti ambako kuna vijiji vitano na visiwa katika Wilaya ya Mkuranga, vijiji vitatu na Mafia vijiji viwili.

“Vijiji hivi ambavyo bado havijapata umeme tayari mpango umeandaliwa, vitafikishiwa umeme wa nishati mbadala kupitia miradi ya off-grid,” alisema.

Mhandisi Olotu alisema Mkoa wa Pwani una vitongoji 2,045 kati ya hivyo, vitongoji 1,135 ambavyo ni asilimia 55.6 vimepata huduma ya umeme.

“Mkandarasi tunayemtambulisha leo atatekeleza mradi katika vitongoji 135 ikiwa na maana ya vitongoji 15 kwa kila jimbo katika majimbo yote tisa ya Mkoa wa Pwani kwa gharama ya Shilingi 14,983,763,390. Aidha vitongoji 775 vilivyobaki vitaendelea kupatiwa umeme kulingana na upatikanaji wa fedha,” alisema.

Mhandisi Olotu alisema REA inatekeleza miradi kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika na kwamba utambuzi wa vitongoji hivyo ulifanywa kwa kushirikisha wabunge wa majimbo yote tisa mkoani humo. 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya