Monday, December 23, 2024
spot_img

DAR ES SALAAM MPYA YA 711 KAWE YAJA 2026

MAKALA YA MTANGAZAJI

TASWIRA ya Jiji la Dar es Salaam itabadilika kabisa ifikapo April, 2026 baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi unaofahamika kwa jina la 711 Kawe.

Mradi wa 711 Kawe unamilikiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na utakapokamilika utabadili mandhari ya makazi katika eneo la Kawe na Jiji la Dar es Salaam kwa ujumla na pia utatoa nafuu na fursa kwa maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuishi kwenye nyumba zenye mandhari ya ubora wa hali ya juu.

Pia kukamilika kwa mradi huu wa 711 Kawe kutaboresha hadhi ya wakazi watakaopata fursa ya kuishi kwenye nyumba hizo na hapo NHC litakuwa limetekeleza lengo lake kuu la kuhakikisha upatikanaji wa makazi bora kwa watanzania.

Ifahamike kuwa majukumu ya NHC ni pamoja na kujenga nyumba za makazi na majengo mengine kwa ajili ya kuuza, kujenga majengo kwa ajili miradi rasmi, kutoa vifaa vya ujenzi, kusimamia biashara ya nyumba na majengo pamoja na shughuli nyingine zilizoidhinishwa na Serikali.

Katika utekelezaji wa majukumu yake hayo, NHC lilianza ujenzi wa nyumba za makazi wa 711 Novemba, 2014 lakini ulisimama mwaka 2018. Jina la mradi huu lilitokana na viwanja vya awali vilivyokuwa vinamilikiwa na NHC ambavyo ni namba 711 na 712.

Mradi huu wa makazi unajumuisha nyumba 422 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo nane yenye ghorofa 18 kila moja. Nyumba za 711 Kawe zimegawanywa katika makundi manne ili kukidhi mahitaji ya makundi yote wa wananchi.

Kwanza ni nyumba zenye vyumba viwili vya kawaida ambazo zipo 24, nyumba za vyumba vitatu 382, kati ya hizo 254 ni za kawaida na 128 ni za kifahari na zipo zenye vyumba vinne; hizi ni za kifahari na zipo 16.

Kila nyumba inayojengwa kwenye mradi huu inajitosheleza kwa huduma muhimu kama sebule, eneo la kulia chakula, maliwato ya wageni na jiko kubwa la kisasa. Pia kuna maegesho ya magari, sehemu za michezo, maeneo ya mbio za riadha na baiskeli, club house na eneo maalumu la kukusanya taka.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah

Utekelezaji wa mradi huu ambao gharama yake ni Shilingi bilioni 169.9 unaendelea kwa kasi kubwa sasa baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa idhini kwa NHC kukopa ili kuukamilisha baada ya kusimama mwaka 2018 na unatarajiwa kukamilika April, 2026.

Uamuzi wa Rais Samia ambao kwa hakika ni uamuzi wa kijasiri kwa kuchukua hatua za makusudi kuendeleza mradi wa 711 Kawe unaingia katika shajara ya Taifa inayorekodi miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali kwa faida ya wananchi.

711 Kawe utatoa suluhisho la kisasa na nafuu la makazi, utasaidia kupunguza upungufu wa nyumba, kupunguza msongamano na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya eneo la Kawe na pia umma utapata manufaa makubwa kwa kuwa na miundombinu iliyoboreshwa, hali bora za kuishi na ongezeko la thamani ya mali litakaloletwa na mradi huu.

Kwa NHC ambalo limesimamia vema majukumu yake kama yalivyoainishwa hapo juu tangu kuanzishwa kwake na hasa kushika usukani wa sekta ya ujenzi wa nyumba za makazi katika Jiji la Dar es Salaam ambalo lina majengo makubwa na ya kisasa ya kuishi; kukamilisha utekelezaji wa mradi wa 711 Kawe kutaifanya Tanzania kuwa na sura mpya.

NHC linatambua changamoto zinazowakabili watanzania walio wengi wanaoishi kwenye nyumba za kupanga kutokana na tofauti ya kipato; linatambua kuwa baadhi ya changamoto hizo ni wapangaji kutodumu kwenye nyumba hizo kwani hulazimika kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya muuda mfupi.

Kwa kutambua hilo NHC limekuwa likibeba jukumu lake kwa ukamilifu la kutoa suluhisho la upatikaniji wa nyumba bora za kupanga kwa haraka, rahisi na kwa gharama nafuu.

Ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi wa 711 Kawe sasa unaendelea

Tayari NHC imeishakusanya Shilingi bilioni 2.9 za mauzo ya nyumba kwenye mrdi wa 711 Kawe huku kasi ya mauzo ikizidi kuongezeka siku hadi siku za utekelezaji wa mradi.

Mwitikio wa wateja wa ndani na nje ya nchi wa kuwekeza kwenye mradi huu ni mkubwa na NHC linawahamasisha watanzania wote, wakiwamo Diaspora kuchangamkia fursa ya kuwekeza kwenye majengo ya 711 Kawe kwa kuwasiliana na Ofisi za Shirika au kupitia tovuti www.nhctz.com.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya