RIPOTA PANORAMA
MAHAKAMA ya Rufaa imetoa uamuzi kuhusu rufaa ya kupinga vifungu vya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai vinavyoruhusu watu kushtakiwa kwenye mahakama ambazo hazina mamlaka ya kuzisikiliza.
Taarifa iliyotolewa Julai 27, 2024 na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) jijini Dar es Salaam ilieleza kuwa uamuzi wa rufaa hiyo ulitolewa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Jaji Kingwele.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Jaji Kingwele alisema jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu walikosea wao kama wao kumpangia jaji mmoja kati yao kusikiliza pingamizi ambalo uamuzi wake ilikuwa kutupilia mbali kesi ya Olengurumwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mahakama ya Rufaa iliamua kuwa, utaratibu sahihi endapo kuna pingamizi limewasilishwa mahakamani, Jaji Kiongozi au Jaji Mfawidhi ndiyo wanaopaswa kupanga jaji wa kusikiliza pingamizi lakini si majaji wenyewe kuamua nani wa kusikiliza kati yao.Ā
āMahakama ya Rufaa kupitia uamuzi wake huo wa leo imeelekeza kesi hiyo irudi tena Mahakama Kuu kwa ajili ya kupangiwa jaji wa kusikiliza pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mwaka 2019 kuwa kesi hiyo inafanana na kesi iliyowahi kuamuliwa miaka ya nyuma (kesi ya Galeba)
āKesi hiyo ilisikilizwa Julai 9, 2024 mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa. Majaji hao ni Jaji Lameck Mlacha, Jaji Augustine Mwarija na Jaji Sam Rumanyika,ā inasomeka taarifa hiyo.Ā
Kesi ya kupinga washtakiwa kushtakiwa kwenye mahakama ambazo hazina mamlaka ilifunguliwa na Mtetezi wa Haki za Binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mwaka 2021.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Eliezer Feleshi
Ilisikilizwa Julai 9, 2024 katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania, jijini Dar es Salaam mbele ya jopo la majaji watatu ambao ni Jaji Rumanyika, Jaji Mwarija na Jaji Mlacha.
Rufaa iliyotolewa uamuzi na jaji Mwangwele inatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala ya Dar es Salaam uliotolewa mwaka 2020 ambapo ilitupilia mbali kesi hiyo kwa misingi kwamba aina ya maombi na kiini cha msingi katika maombi hayo tayari ilikwisha amriwa katika mashauri ya awali (Res Judicata)
Kesi hiyo ilikuwa inapinga vifungu vya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai vinavyoruhusu washtakiwa kushtakiwa kwenye mahakama za chini ambazo hazina mamlaka ya kuzisikiliza kesi (committal Proceedings).
Vifungu vilivyolalamikiwa ni namba 178, 243, 244, 245, 246, 247, 248, 249, 250, 256, 257,258 na 259 vya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA) kuwa vinakiuka Katiba na haki za binadamu.
Mifano iliyotolewa ni haki ya kusikilizwa kwa usawa na usawa mbele ya sheria ambazo zipo katika Ibara ya 13 (1) (2) na (6) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Katika rufaa iliyokatwa na Olengurumwa, kulikuwa na hoja mbili ambazo ni; Mahakama Kuu ilikosea kutupilia mbali kesi hiyo kwa kigezo kuwa kiini na aina ya kesi hiyo ilikwisha amriwa katika kesi ya Galeba.
Kwamba kesi ya Galeba ilipinga vifungu viwili tu, wakati kesi ya Olengurumwa inapinga vifungu 13 vya CPA.
Hoja ya pili ni jopo la majaji wa Mahakama Kuu walikosea wao kama wao kumpangia jaji mmoja kati yao ili kusikiliza pingamizi lililotoa uamuzi wa kesi hiyo kutupwa kinyume na utaratibu ambapo ilitakiwa Jaji Kiongozi ndiye apange jaji mmoja kusikiliza pingamizi.