Friday, May 30, 2025
spot_img

MTUNZA FUNGUO ZA AL – KAABA AFARIKI DUNIA

MASHIRIKA YA HABARI YA KIMATAIFA

MTUNZA funguo za eneo takatifu kwa waumini wa dini ya kiislamu, Dk. Saleh bin Zainul Abedin Al Shebi amefariki dunia juzi, Juni 30, 2014 nchini Saudi Arabia akiwa na umri wa miaka 77.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali vya kimataifa, Dk. Saleh alikuwa mrithi wa 109 wa familia ya Al Shebi aliyekuwa na jukumu la kutunza ufunguo wa kuingia eneo hilo takatifu la Waislamu.

Kwa karne nyingi, familia ya Dk. Saleh ndiyo imekuwa na jukumu la kutunza ufunguo wa Al Kaaba na Dk. Saleh mwenyewe alipewa jukumu la kutunza funguo huo baada ya kifo cha mjomba wake, Abdul Qadir Taha Al Shebi kilichotokea mwaka 2013.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeripoti kuwa Dk Saleh alikuwa msomi aliyebobea wa masomo ya dini ya kiisalamu akiwa na shahada ya udaktari (PHd) aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Umm Ul Qura.

Dk. Saleh bin Zainul Abedin Al Shebi

Alizaliwa mwaka 1947 katika Mji Mtakatifu wa Mekka na wakati wa uhai wake alipata kufundisha Chuo Kikuu alichosoma cha Umm Ul Qura kwa miaka mingi kama mhadhiri na amefanya utafiti na kuchapisha vitabu vingi vinavyohusu dini ya Uislamu.

Eneo Takatifu la Al Kaaba lina mlango mmoja tu unaoitwa Bab  e Kaaba wenye urefu wa mita 2.13 kutoka kwenye sakafu ya Msikiti wa Al Haram na mlango huo upo karibu na ukuta wa Kaskazini Mashariki ya Al Kaaba na pia karibu na jiwe jeusi; mahali inapoanzia Tawaf.

BBC imefanya mahojiano na mwana historia wa dini ya Kiislamu, Ahmed Adan kuhusu historia ya ufunguo wa Al Kaaba aliyeeleza kuwa wakati Mtume Mohammad anazaliwa, majukumu ya familia yake ya Bani Hashim yalikuwa kusimamia kisima za Zamzam na ufunguo wake huku ufunguo wa Al Kaaba ukitunzwa na Usman bin Talba.

Kwa mujibu wa mwana historia huyo ni Mtume Muhammad aliyemweleza Uthman bin Talha kuwa siku zinakaribia za ufunguo huio kuwa mikononi mwake.

Historia ya dini ya kiislamu inaonyesha kuwa baada ya kutekwa kwa Mji wa Makka, ufunguo wa Al Kaaba ulichukuliwa kutoka kwa Uthman bin Talha lakini ulirudishiwa kwake kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Kwamba Mtume Muhammad mwenyewe alimpatia Usman bin Talha ufunguo huo na tangu wakati huo familia yake ndiyo imekuwa na jukumu la kuutunza; kizazi hadi kizazi.

Inaelezwa kuwa wakati Mtume Muhammad alipokuwa akimkabidhi Usman bin Talha ufunguo wa Al Kaaba alitamka kwamba utabaki kwake na hakuna mtu atakayeweza kuuchukua isipokuwa mtu dhalimu.  

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya