Wednesday, June 25, 2025
spot_img

MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI YATAJWA

RIPOTA PANORAMA

MABADILIKO makubwa ya Baraza la Mawaziri yanatabiriwa kufanywa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wowote  baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 15 wa Bunge unaofikia ukingoni mwishoni mwa wiki hii.

Mabadiliko hayo yanatabiriwa kuwagusa mawaziri ambao kasi ya utekelezaji wa majukumu yao haiendani na tamaa na azma ya Rais Samia ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya serikali inayoiongoza pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 ambacho yeye ni mwenyekiti wake 

Wachambuzi na wafuatiliaji wa mambo wanaeleza kuwa katika mabadiliko hayo, Rais Samia anaweza kuwabadilisha baadhi ya mawaziri wenye uwezo mkubwa waliouthibitisha katika utendaji wao kwenye wizara wanazoongoza sasa na kuwapeleka kwenye wizara nyingine zinazohitaji usimamizi madhubuti; lengo likiwa kuongeza ufanisi wa kiutendaji.

Mobhare Matinyi

Inaelezwa kuwa mabadiliko hayo ni mwendelezo wa mabadiliko ambayo amekuwa akiyafanya siku za hivi karibuni kwenye idara na taasisi nyeti za Serikali yakilenga kupanga vizuri safu ya wasaidizi wake na kuimarisha utendaji kazi serikalini.

Aidha, inaelezwa kuwa Rais Samia anaweza kuwashangaza wengi kwa kufanya mabadiliko yatakayogusa wizara nyeti ikiwa ni pamoja na kuwaacha pembeni baadhi ya mawaziri vigogo na kuingiza sura mpya kwenye baraza lake la mawaziri na kuwapandisha wengine.

Hivi karibuni, Rais Samia amefanya mabadiliko makubwa ya wasaidizi wake wa Ikulu ambayo pia yalimgusa aliyekuwa. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus aliyemteua kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Zuhura Yunus

Mabadiliko mengine yaliyofanywa na Raisi Samia katika nafasi nyeti yalimgusa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi aliyepangiwa majukumu mengine huku nafasi yake ikichukuliwa na Thobias Makoba ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Tangu alipoingia madarakani, Rais Samia ambaye mtindo wake wa uongozi ni wa ushirikishaji na uelekezaji na zaidi uvumilivu kwa wateule wake akilenga kuwapa uwanda mpana wa utekelezaji majukumu yao na kusahihisha makosa ya kawaida kiutendaji, amekuwa akifanya mabadiliko ya nafasi mbalimbali za viongozi kwa kuimarisha maeneo ambayo hayafanyi vizuri na kuwatupa pembeni wale ambao mwenyewe amepata kusema ‘wakimzingua na yeye anawazingua.’

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya