Thursday, July 17, 2025
spot_img

RAIS SAMIA AMWAGA NOTI TFC, SASA KUJIENDESHA KIBIASHARA

RIPOTA PANORAMA

SERIKALI imeipatia Kampuni ya Mbolea (TFC) mtaji wa Shilingi 110 bilioni katika mwaka wa fedha 2023/2024 ambazo zimeiwezesha kujiendesha kibiashara.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Samuel Mshote hivi karibuni kuhusu mwenendo wa kampuni hiyo, ilieleza kuwa utendaji wake sasa umeimarika sambamba na kuimarishwa kwa menejimenti ambayo imeongezewa watumishi wenye uwezo na ujuzi wa kiutendaji.

“Sasa tunakwenda vizuri. Kampuni inapata mafanikio makubwa kiutendaji na hii ni kwa sababu ya dhamira ya Rais Samia mwenyewe ambaye katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 ametupatia TFC Shilingi 110 bilioni za mtaji ili tuweze kujiendesha kibiashara.

“Fedha hizo zilitolewa kwa awamu, kwanza tulipokea Shilingi 40 bilioni kutoka Bajeti Kuu ya Serikali, kisha tukapewa Shilingi 70 bilioni kutoka katika miradi ya maendeleo.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea (TFC) Samuel Mshote

“Rais Samia ameimarisha Bodi ya Wakurugenzi kwa kuteua Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, menejimenti sasa ina watu wenye uwezo na ujuzi ndiyo maana ukiangalia mwenendo wa utendaji wa kampuni unaona mafanikio ni makubwa,” alisema Mshote katika taarifa yake.

Akizungumzia mafanikio yaliyofikiwa na kampuni hiyo anayoiongoza, alisema kwa mwaka 2023/2024 imeweza kununua tani 4500 za mbolea ambayo ilisambazwa kwa wakulima kwa  wakati, wakiwemo ambao walikuwa hawapati mbolea kabla ya kuimarishwa kwa kampuni hiyo.

Mshote alisema TFC imeishakamilisha taratibu za manunuzi ya tani 75,000 za mbolea na shehena ya kwanza ya mbolea hiyo, tani 25,000 imekwishapokelewa huku tani 49,000 zikitarajiwa kuingia wakati wowote.

“Tunachokifanya sasa ni kuhahakisha mbolea hii inasambazwa na kuwafikia wakulima kwa wakati na tunaweka mawakala wa kutosha nchi nzima wa kusambaza mbolea kwa wakulima.

Shehena ya Mbolea

“Tunashirikiana kwa karibu sana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) ambayo imesajili vyama vya ushirika 29 vinavyosaidia usambazaji wa mbolea kwa wakulima lakini pia tunawatumia wenzetu wa Halmashauri za Miji ambao wana maghala. Wanatusaidia kufikisha mbolea kwa wakulima,” alisema.

Alisema takwimu zilizopo zinaonyesha ufanisi mkubwa wa usambazaji mbolea katika mikoa 17 ambako mbolea iliwafikia wakulima kwa wakati na mpango wa TFC kwa sasa ni kuwafikishia wakulima mbolea kwa wakati kwenye mikoa yote 26 nchini.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya