Sunday, September 7, 2025
spot_img

MIKAKATI MIZITO TFC KUINUA SEKTA YA KILIMO

RIPOTA PANORAMA

KAMPUNI ya Mbolea (TFC) imepanga mikakati mizito katika mwaka wa fedha 2024/2025 itakayowezesha azma ya Serikali kuinua Sekta ya Kilimo.

Hayo yameelezwa na Mkutugenzi Mkuu wa TFC, Samuel Mshote hivi karuibuni alipokuwa akizungumzia mafanikio ya kampuni hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ya uhai wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Alisema ili kuwezesha wakulima kulima kilimo chenye tija na kupata mazao ya kutosha, TFC imepanga kuanza kutumia usafiri wa reli kusafirisha mbolea kwa treni ya kisasa ya mwendo kasi ili kuongeza wigo wa kusambaza mbolea kwa wakulima nchi nzima.

“Sasa tutatumia reli badala ya barabara kusambaza mbolea kwa wakulima nchi nzima ili iwafikie kwa wakati, tunaamini tukitumia reli tutaweza kusafirisha shehena ya kutosha ya mbolea na itawafikia wakulima wengi kwa wakati,” alisema.

Aliutaja mkakati mwingine kuwa ni kujenga kiwanda cha mbolea hapa nchini, hatua ambayo itapunguza gharama za kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi na pia itatoa ajira kwa watanzania.

“Tunataka tuanze kuzalisha mbolea na kuichanganya hapa hapa nchini. Tupo kwenye hatua ya kutafuta eneo tutakalojenga kiwanda hicho. Tunatafuta eneo Mkoa wa Dar es Salaam na Tanga. Tunataka tujenge kiwanda cha kuzalisha tani 120 za mbolea kwa saa. Tunataka tutosheleze mahitaji ya ndani ya tujielekeze kwenye soko la nje ya nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea (TFC) Samuel Mshote

“Tunakusudia kuboresha maghala yetu ya kuhifadhia mbolea. Hivi sasa tuna kanda sita za mauzo na tuna maghala saba ambayo yana uwezo wa kuhifadhi tani 100,000 za mbolea, haya tutayaongezea uwezo,” alisema Mshote.

Alisema wataalamu wa TFC sasa wanakuna vichwa ili kuja na mipango mipya ya namna ya kuhifadhi mbolea na pembejeo na kwamba mezani kwake tayari umewasilishwa mpango wa kuingia makubaliano na kampuni kubwa zenye uwezo na ujuzi wa uhifadhi wa mbolea na pembejeo.

“Wataalamu wangu tayari wamekwishawasilisha mpango wa kuingia makubaliano na kampuni kubwa zenye uwezo na ujuzi wa kuhifadhi mbolea na pembejeo lakini pia kampuni hizo zina uwezo mkubwa wa uzalisha mbolea.

“Tunangalia kwa umakini mkubwa kampuni inayofaa, lakini mapendekezo yanataja kampuni kutoka Nchi za Saudi Arabia, Urusi lakini pia kuna majadiliano yanaendelea na kampuni moja ya Qatar ambayo ina uwezo mzuri sana wa uzalishaji mbolea,” alisema.

Alisema hayo yakifanikiwa, TFC itakuwa inatembea kwenye unyayo wa Rais Samia Suluhu Hssaan kuelekea kwenye azma yake za Sekta ya Kilimo kuchangia asilimia 10 katika pato la Taifa ifikapo mwaka 2030.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya