Tuesday, December 24, 2024
spot_img

NAIBU WAZIRI MAHUNDI KUFUNGUA BARAZA LA 42 LA UTAWALA LA UMOJA WA POSTA AFRIKA

MWANDISHI WETU, WHMTH

Arusha 

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU), unaofanyika Makao Makuu ya Ofisi za Umoja huo, Jijini Arusha Juni 11 hadi 12, 2024.

Mhandisi Mahundi atafungua mkutano huo Juni 11, 2024 na utajadili maazimio na taarifa za vikao vya kamati za wataalamu wa masuala ya posta vilivyoanza Juni 3, 2024; vilivyojadili masuala mbalimbali yanayohusu fedha na utawala, mkakati, sera na kanuni, pamoja na uendeshaji na teknolojia.

Mkutano huu utahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi wanachama wa PAPU pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Posta kutoka barani Afrika na wajumbe wa Sekretarieti ya Umoja wa Posta Duniani.

Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika ni jukwaa muhimu kwa maendeleo ya Sekta ya Posta barani Afrika, likiwa na jukumu la kuziunganisha nchi wanachama kupata fursa, kujadili changamoto na kutafuta suluhu endelevu kwa ajili ya kuboresha huduma za posta katika nchi wanachama 45.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya