Monday, December 23, 2024
spot_img

IBANDA – KYERWA PARADISO YA NDEGE

RIPOTA PANORAMA

HIFADHI ya Taifa ya Ibanda – Kyerwa ni makazi ya ndege wengi wa aina mbalimbali waliotapakaa duniani.

Ni rahisi kuona aina tofauti tofauti za ndege waliopo duniani hususan ukanda wa Afrika Mashariki wakiwemo wanaoishi kwa kuhama kutoka eneo moja kwenye eneo jingine.

Uchunguzi wa kitaalamu wa aina za ndege zilizopo kwenye hifadhi hiyo uliofanywa hivi karibuni na watafiti wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wale wa Hifadhi ya Taifa ya Ibanda – Kyerwa imeonyesha kuwa hifadhi hiyo ina aina 188 za ndege.

Mkuu wa Hifadhi ya Ibanda – Kyerwa, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Dk. Fredrick Marco Mofulu katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu mwenendo wa utalii pamoja na vivutio vya kipekee vya utalii vilivyo katika hifadhi hiyo, alisema ina aina tofauti za makazi ya wanyama na ndege wa msituni na majini, uwanda wa Savana, tambarare, vilima, mabonde na mito.

Mkuu wa Hifadhi ya Ibanda – Kyerwa, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Dk. Fredrick Marco Mofulu

“Kuna aina nyingi za uoto wa asili kuanzia nyika za miti ya migunga, milima na mabonde, mito na tambarare zinazoifanya hifadhi hii kuwa na mandhari nzuri na ya kuvutia inayowapa watalii fursa nzuri ya kujionea aina tofauti za uoto wa asili.

“Lakini pia Hifadhi ya Taifa ya Ibanda – Kyerwa ina kitu kingine cha zaidi, nacho ni makazi yanayofaa kwa aina mbalimbali za ndege. Utafiti uliofanywa hivi karibuni na watafiti wetu umeonyesha kuwa hifadhi hii ina spishi 188 za ndege na utafiti huu ulifanyika wakati wa kiangazi.

“Tunatarajia kuendelea kugundua aina nyingine zaidi za spishi lakini naweza kukwambia kuwa hapa Hifadhi ya Taifa ya Ibanda – Kyerwa ndipo unapoweza kumuona njiwa mwenye shingo ya pete na tuna uhakika kuwa katika uchunguzi utakaofanyika msimu wa mvua, kati ya Oktoba na Aprili, spishi zaidi zitagunduliwa kwa sababu zipo ambazo huwa zinahama hama lakini wakati wa mvua hupendekea kuishi kwenye eneo hili,” alisema Kamishna Msaidizi Dk. Mofulu.

Hifadhi ya Taifa ya Ibanda – Kyerwa ni moja ya hifadhi zilizopandishwa hadhi miaka michache iliyopita na imebainika kuwa na vivutio vya kipekee.

Ilitangazwa kupandishwa hadhi kuwa Hifadhi ya Taifa kutoka pori la akiba lililoanzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1971, kwenye gazeti la serikali la Julai 5, 2019 ikiwa wa eneo la kilomita 294.

Ndege aina ya Thrush wa kiafrika

Ndege aina ya kresrel wa kijivu

Ndege aina ya taji wa pembe

Ndege mzeituni

Ndege mkuki wa klaa’s

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya