Tuesday, June 17, 2025
spot_img

ICC YAWAWINDA BENJAMIN NETANYAHU, YOAV GALLANT

MASHIRIKA YA KIMATAIFA

MWENDESHA Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), Karim Khan ametangaza kusudio la ofisi yake la kuwakamata na kuwafikisha mahakamani Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi, Yoav Gallant kwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Pamoja nao, ametangaza pia kusudio la ofisi yake la kuwakamata viongozi watatu wa kundi la kigaidi la Hamas, wakiwamo Ismail Haniyeh na Mohammed Dief.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), jana lilimkariri Khan akieleza kuwa ICC imejiridhisha kuwa zipo sababu za kukamatwa kwa Netanyahu, Gallant na viongozi wakuu wa Hamas.

Alisema Netanyahu, waziri wake wa ulinzi na viongozi wa juu wa Hamas wanawajibika kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ulioanza Oktoba 7, 2023.    

ICC yenye makao makuu yake The Hague, Uholanzi imekuwa ikichunguza hatua zinazochukuliwa na Israel kwenye maeneo ya Palestina yanayokaliwa na Israel.

Kuhusu viongozi wa kundi la kigaidi la Hamas alisema nao wamekuwa wakichunguzwa kwa vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na kundi hilo dhidi ya raia wa Israel.

Khan aliwashutumu viongozi wa Hamas kwa kutekeleza vitendo vya uhalifu kwa kuangamiza watu, mauaji, utekaji nyara, ubakaji, unyanyasaji wa kingono na mateso dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.

Majaji wa  Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita sasa wanasubiriwa kuamua kama kuna ushahidi wa kutosha ili kutoa hati ya kukamatwa kwa viongozi hao.

Previous article
Next article

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya