Monday, December 23, 2024
spot_img

IDRIS SULTAN ANOGESHA MSIMU WA TATU WA BRIDGERTON

JOSEPH SHALUWA

STAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha ujio mpya wa tamthilia ya Bridgerton, katika onesho kabambe lililowakusanya nyota daraja la kwanza kutoka Afrika Mashariki na Bara la Afrika kwa ujumla.

Idris Sultan

Onesho hilo lilifayika, Mei 4, mwaka huu nchini Afrika Kusini, ambapo Netflix, waandaaji wa series hiyo walizindua msimu wa tatu wa Bridgerton.

Msimu wa tatu wa Bridgerton unatarajiwa kurushwa na Netflix na kushuhudiwa na ulimwengu mzima Mei 16, mwaka huu ambapo itaruka sehemu ya kwanza na sehemu ya pili Juni 13, mwaka huu.

Katika onesho hilo, lililopewa jina la ‘Regency Era Splendor: Into The Spotlight’ lilihudhuriwa na mastaa wakubwa kutoka Kenya, Tanzania, (Idris), Nigeria, Ghana, Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini, wakiongozwa na Adjoa Andoh (ambaye amecheza kama Lady Aga kwenye Bridgerton) akiwa kama mgeni wa heshima.

Catherine Kamau

Mkali wa kurapu free style, kutoka Afrika Kusini ambaye amependekezwa kwenye Tuzo za Grammy, Musa Keys naye aliungana na mastaa wenzake katika hafla hiyo.

Mbali na Idris, mastaa wengine kutoka Afrika Mashariki – Kenya walioalikwa katika onesho hilo la kijanja ni pamoja na komediani na mtayarishaji maudhui, Elsa Majimbo.  

Wengine kutoka ardhi ya William Ruto ni staa wa filamu Catherine Kamau (Kate), Amina Abdi Rabar na waigizaji mahiri: Manasseh Nyagah na Jackie Matubia. 

Musa Keys

Wanamitindo maarufu wa Nairobi: Brian Babu na Lady Mandy pia walihudhuria, ambapo kwa pamoja walihusika katika kubuni na kutengeneza mavazi ya mastaa waliohudhuria.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya