Monday, December 23, 2024
spot_img

WAHITIMU UDSM FIVE CLASS 2007 KUJADILIANA FURSA ZA KIUCHUMI

MWANDISHI MAALUMU, DAR

WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) five Class 2007 wanatarajia kukutana jijini Dar es Salaam kubadilishana mawazo na kushirikishana fursa mbalimbali za maendeleo.

Wanafunzi hao wa Kitivo cha Infirmatics and Virtual Education (FIVE) ambayo sasa inajulikanana College of ICT (CoICT), pamoja na mambo mengine watabadilishana mawazo na kupanga mikakati ya maendeleo ya uchumi.

Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog leo, April 30, 2024 jijini Dar es Salaam, kiongozi wa wahitimu hao, Frank Gwaluma amesema kikao hicho kitafanyika The Deck Kitchen & Bar iliyopo Masaki karibu na Kambi ya Jeshi Mei 24, mwaka huu.

Amesema lengo la kikao hicho ni kukumbushana walikotoka na kubadilishana mawazo ikiwa ni pamoja na kushirikishana fursa za maendeleo na uchumi.

“Ni kikao cha kawaida tumekiandaa sisi tuliokuwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Facult ya Informatics and Virtual Education (FIVE) kwa sasa College of ICT (CoICT).

bAADHI ya wahitimu waliosoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Facult ya Informatics and Virtual Education (FIVE) kwa sasa College of ICT (CoICT) wanaotarajia kukutana April 30, 2024 jijini Dar es Salaam kujadiliana fursa za kiuchumi,.

“Tukizingatia ni muda mrefu umepita hatujakutana hivyo tumeona huu ni wakati muafaka kwetu kujumuika, kufurahi pamoja na kujadiliana fursa za maendeleo, hili ndilo lengo letu hasa.

“Nichukue fursa hii kuwakaribisha wenzetu wote ambao tulisoma pamoja lakini kwa sababu mbalimbali hatuna mawasiliano nao wajue tupo na tunawahitaji sana wajumuike nasi” amesema Gwaluma.

Kuhusu mgeni rasmi, Gwaluma amesema wanatarajia kuwa na baadhi ya walimu waliowafundisha chuoni hapo na humo ndipo atapatikana mgeni maalumu.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya