Monday, December 23, 2024
spot_img

‘JANGA’ LA KITITA KIPYA CHA BIMA YA AFYA

RIPOTA PANORAMA

KITITA kipya cha Bima ya Afya (NHIF) kilichopitishwa kwa kutumia kiwango cha chini cha orodha ya bidhaa kuamua huduma ya dawa katika kitita hicho, itatudumaza utoaji huduma hususan kwenye vituo vya afya vya binafsi.

Kitita hicho kipya cha Bima ya Afya kitasababisha ubaguzi kwa sababu kitawahitaji wagonjwa kuanza kugharamia dawa na huduma kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

Haya yameelezwa kwenye maoni ya maboresho ya kitita cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya mwaka 2023, yaliyotolewa na Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) kwa Wizara ya Afya iliyoomba maoni ya wadau kukiboresha.

PST chini ya rais wake, Fadhil Hezekiah na Katibu Mkuu, Benson Katundu kimeeleza kuwa baada ya kupitia kitita kipya na kufuatilia maoni ya wanataaluma na famasi, kimejiridhisha kwamba mabadiliko yaliyofanywa kwenye kitita ni makubwa sana.

Chama hicho kimeeleza kuwa kuhusishwa kwa bei na aina ya huduma, dawa na bidhaa nyingine za afya kwenye mabadiliko hayo ni sawa na kuunda kitita kipya hivyo kwa mantiki hiyo, utaratibu uliotumika kufanya mabadiliko siyo sahihi.

PST kimetaja upungufu kiliobaini kwenye mabadiliko yaliyofanywa kuwa ni rejea ya kitita zaidi katika orodha ya taifa ya dawa muhimu (NEMLIT) iliyotumika kwenye mabadiliko ipo kwenye maboresho kwani imepitwa na wakati hivyo haikuwa sahihi kuitumia kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya kimatibabu.

“NEMLIT ni minimum standard (kiwango cha chini). Inakuwa na orodha ya dawa chache kutokana na epemiolojia ya magonjwa, sera na hali ya uchumi kwenye nchi husika. Hutumika kama kigezo cha chini kwa nchi kujipima wakati wa kufanya tathimini ya upatikanaji wa dawa.

“Pia kuzipa nafasi hospitali, taasisi binafsi za misaada na mashirika mengine kupanga na kuelekeza rasilimali katika kuhakikisha wanawekeza au kuweka bajeti kulingana na dawa zilizopo kwenye orodha ya taifa.

“Kutumia kiwango cha chini cha orodha ya bidhaa kuamua huduma za dawa katika kitita cha Bima ya Afya kutadumaza huduma kwa wateja wengi hasa hasa katika vituo binafsi kutakakohitaji kuchangia baadhi ya gharama ya dawa na huduma. Jambo hili litaturudisha nyuma kipindi wateja wa NHIF walikuwa wakibaguliwa,” inasomeka sehemu ya maoni hayo na sehemu nyingine inasomeka hivi;

“Aidha, NEMLIT ina dawa moja moja (monotherapy) kama mwongozo ila katika uhalisia, magonjwa mengi hasa NCDs yanalazimisha mgonjwa kuhitaji dawa zaidi ya moja jambo ambalo kwa sasa itapaswa mgonjwa apewe dawa moja moja na kumfanya kuwa na dawa nyingi. Hii itapunguza uzingatiaji wa matibabu na inaweza kusababisha ongezeko la complications (matatizo).

Dawa aina ya Hydrochlorothiazide inayohitaji kuongezewa dawa nyingine ili kuiwezesha kufanya kazi kwa ufanisi kwenye mwili wa binadamu

“Kadhalika kwa antibiotics, kuna baadhi zinahitajiana ili kuongezeana uwezo vinginevyo husababisha ongezeko la usugu wa vimelea.”

Wafamasia hao wanaandika maoni yao wakitoa mfano wa dawa zinazohitajiana kuongezena uwezo kuwa ni Amlodipine na hydrochlorothiazide na nyingine ni Losartan na Hydrochlorothiazide.

Wakiendelea, wanasisitiza kuwa NEMLIT inayotumika sasa imepitwa na wakati na iko kwenye maboresho hivyo siyo sahihi kutumika wakati huu wa mabadiliko makubwa ya kimatibabu na kwamba kutumika kwake kumesababisha bidhaa nyingi zenye ufanisi mkubwa kuachwa kwenye kitita kipya ncha NHIF.

   

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya