Monday, December 23, 2024
spot_img

NHIF HAITASIMAMA KWA MABADILIKO YA BEI YA KITITA – PST

RIPOTA PANORAMA

CHAMA cha Wafamasia Tanzania (PST), kimeeleza kuwa mabadiliko ya bei ya kitita cha Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), hayataiwezesha kusimama imara.

PST kimeeleza haya kwenye maoni yake ya maboresho ya kitita cha NHIF kama kilivyoombwa na Wizara ya Afya Machi 13, 2024.

Taarifa ya PST kuhusu maboresho ya kitita cha NHIF iliyotolewa mwishoni mwa mwezi Machi ikiwa imeidhinishwa na rais wake, Fadhil Hezekiah na Katibu Mkuu, Benson Katundu ambayo Tanzania PANORAMA Blog imeiona, imeeleza kuwa chama hicho kimejiridhisha kwamba bei za huduma na bidhaa za afya haikuwa miongoni mwa changamoto za mfuko.

Kwamba, kwa kuzingatia hilo, hakuna mantiki kwenye uamuzi uliochukuliwa wa mabadiliko ya bei za vitita vya NHIF kwa kuzingatia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2021/2022 iliyoonyesha changamoto za mfuko huo.

PST kimeeleza kwenye taarifa yake kuwa bei za bidhaa kama zilivyo kwenye kitita cha awali cha NHIF haikutajwa na CAG kuwa miongoni mwa changamoto za mfuko hivyo kinachotakiwa sasa ni kufahamu chanzo cha changamoto za NHIF ili kupata majibu sahihi na ya kudumu.

“Kwa kuwa changamoto tajwa hapo juu hazikuhusisha bei ya bidhaa, ni wazi kwamba hata bei zikibadilika bila suluhisho la changamoto hizo, kamwe mfuko hauwezi kusimama imara. Maswala ya bei za vifaa hayapaswi kuchukuliwa kwa udharura ili kuepusha makosa kujirudia,” inasomeka sehemu ya taarifa PST.

Chama hicho kimetoa mapendekezo ya muda mfupi matatu na ya muda mrefu matano ambayo yataiwezesha NHIF kukabiliana na wakati mgumu ilionao sasa; na pendekezo la kwanza la muda mfupi ni kulipwa haraka iwezekanavyo fedha za mfuko zilizokopwa.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere

Pendekezo la pili ni fedha za NHIF kutumika kulipia gharama za mfuko zenye tija kwa wanufaika na kwa asilimia zilizopangwa na kwamba upanuzi wa huduma uendane na kasi ya uchumi na kadri kila mtoa huduma ataona uhitaji wa soko.

Pendekezo la muda mfupi la mwisho lililotolewa ni kuchukuliwa hatua kali watu waliobainika kushiriki kufanya udanganyifu kwenye fedha za mfuko wa NHIF.

Kwa upande wa mapendekezo ya muda mrefu, PST imependekeza kuundwa chombo huru cha kusimamia gharama za matibabu nchini na pili; NHIF kuwekeza zaidi kwenye kinga ya magonjwa yanayoambukiza ambayo matibabu yake yanagharimu fedha nyingi.

PST imependekeza pia kufanyika kwa tathimini ya kina ya wanufaika wa hiari ambao hujiunga na NHIF baada ya kugundua wana changamoto ambazo zipo nje ya uwezo wao huku michango yao ikiwa haiendani na huduma wanazotumia.

“Kwa dawa na huduma ghali, kuwe na mpango maalumu wa kushughulika nazo ili zisiharibu ‘graph’ na kuathiri dawa na huduma nyingine. Kwa ngazi zote za ajira, NHIF iajiri wataalamu waliotoka kazini na wana uelewa wa hali ya afya,” yanasomeka mapendekezo mawili ya mwisho ya PST.

Version 1.0.0

Bandeji inayojulikana kwa jina la Elastic adhesive 4cm x 4m ambayo ni moja ya kifaa tiba kilichoondelewa kwenye kitita kipya cha Bima ya Afya

Ripoti ya CAG ya 2021/2022 inaonyesha kuwa NHIF ilipata nakisi ya Sh. 189.65 bilioni kabla ya kodi ambayo chanzo chake kikubwa ni michango ya wanachama kuwa chini ya gharama zilizotumika kwao.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya CAG, gharama za wanachama zilikuwa zikikua kuliko michango yao kwa miaka mitano mfululizo na faida ghafi ilikuwa ikipungua kila mwaka.

CAG anakariri mapendekezo ya watathimini wa NHIF yanayoeleza umuhimu wa kuangalia upya na kubadili baadhi ya masharti ya uanachama wa hiari, kuboresha kanzidata na TEHAMA, kuboresha usimamizi wa watoa huduma za bima ya afya na kutathimini na kusimamisha baadhi ya uwekezaji kama vile mikopo iliyotolewa kwa taasisi za Serikali.

Ripoti ya CAG ya mwaka 2022/2023, pamoja na mambo mengine inaonyesha kuwa mambo ambayo yanaweza kuathiri uhai wa muda mrefu wa NHIF ni mikopo ya Serikali ya Sh. 208 bilioni ambayo haijalipwa inayousababisha mfuko mzigo mkubwa wa kifedha licha ya serikali  kupanga kulipa Sh.180 bilioni katika bajeti ya 2024/2025.

GAG katika ripoti yake ya 2021/2022, pia alionyesha jinsi wafanyakazi wa NHIF walivyokopa Sh 41.42 bilioni bila kuzingatia mahitaji ya sera ya mfuko ya kukopa na kulipa.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya