Thursday, July 17, 2025
spot_img

TPC YATENGA BILIONI 1.4 KURUDISHA KWA JAMII

RIPOTA PANORAMA – Kilimanjaro

 KIWANDA cha Sukari cha TPC kilichopo Mkoa wa Kilimanjaro, kimetenga Shilingi bilioni 1.4 kusaidia maendeleo ya jamii.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha TPC anayeshughulikia utawala, Jafari Ally wakati wa mahojiano yake na Tanzania PANORAMA Blog, hivi karibuni.

Ally alisema kiasi hicho cha fedha kitatumika kuboresha Sekta ya Elimu na hasa kukarabati shule za msingi na sekondari.

“Huu ni mkakati wetu TPC kuboresha uhusiano na jamii inayozunguka kiwanda lakini pia tukiwa sehemu ya Sekta Binafsi, tunafanya hivi kuunga mkono juhusu za serikali kuboresha maisha ya watu wake tukizingatia mazingira mazuri ya uwekezaji iliyotuwekea,” alisema Ally. 

Alisema TPC ni moja ya walipa kodi wkubwa nchini na kinatumia sehemu ya faida inayopatikana kwenye shughuli zake kusaidia shughuli za kijamii kwa wananchi wa vijiji vya jirani na kiwanda.

“TPC tumetoa kipaumbele kusaidia Sekta za Afya, Elimu, Maji na Miundombinu ya Barabara. Kwenye barabara tunakarabati maeneo korofi  na kuyajenga kwa kiwango cha moramu sehemu zinazohitajika.

“Kuhusu elimu tumeanzisha mpango maalumu wa kukarabati shule nne za msingi zilizopo maeneo ya vijjini,” alisema Ally.

Alitaja baadhi ya shule zilizo kwenye mpango huo kuwa ni Shule za Msingi Mikocheni ambayo ukarabati wake umegharimu Sh. milioni 200 na Shule ya Msingi Kiyungi ambayo ukarabati wake umegharimu Sh. milioni 56.

Alisema Shule ya Msingi Arusha itakarabatiwa kwa gharama ya Sh. milioni 60 na ukarabati huo utahusisha vyumba 12 vya madarasa vinavyotumiwa na wanafunzi 400.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Arusha, Suzan Eliahaki alisema kukarabatiwa kwa shule hiyo kongwe iliyojengwa  zaidi ya miaka 50 iliyopita kutaleta manufaa makubwa kutokana na changamoto zilizokuwa zikiwakabiri walimu na wanafunzi hasa kipindi cha masika.

Moja ya majengo ya madarasa ya Shule ya Msingi Arusha lililofanyiwa ukarabati na Kiwanda cga TPC kilichopo Mkoa wa Kilimanjaro. Picha ya juu ni jengo hilo kabla ya kukarabatiwa.

Mwalimu Eliahaki alisema meneo mengine yaliyofanyiwa ukarabati mkubwa ni matundu 20 ya vyoo, stoo na bohari ya shule.

Akizungumzia Shule za Sekondari, Ally alisema TPC imejenga shule mpya ya sekondari ya Chekereni, Weruweru yenye uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 600.

Alisema kabla ya kujengwa kwa shule hiyo, wanafunzi walilazimika kutembea umbali wa kilometa 27 kwenda na kurudi shuleni.

Aidha, Ally alisema TPC inatoa msaada kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaoomba mikopo Bodi ya Mikopo na kupatiwa chini ya asilimia mia moja.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya