Sunday, August 24, 2025
spot_img

‘MADUDU’ YA TFC MBOLEA YA BILIONI 7.9

RIPOTA PANORAMA

KAMPUNI ya Mbolea Tanzania (TFC), imefanya ‘madudu’ ya kutisha kwenye manunuzi ya tani 4500 za mbolea, yenye thamani ya Shilingi bilioni 7,915,794,880.

TFC imenunua mbolea hiyo bila kutangaza tenda, haina nyaraka yoyote iliyoandaliwa na menejimenti kwa ajili ya manunuzi, hakuna kikao chochote kilichoketi kuamua kufanya manunuzi na bila kushirikisha Bodi ya Zabuni.

Hayo yamo kwenye Ripoti ya Mkaguzi wa Ndani wa TFC, Malik Aram ambaye amefanya ukaguzi kwenye  manunuzi, usambazaji na uuzaji wa mbolea hiyo, kuanzia Januari hadi Juni 2023.

Kwa mujibu wa ripoti, TFC ilinunua tani 4500 za mbolea kienyeji huku ikifanya ukiukwaji mkubwa wa sheria ya manunuzi ya umma na pia ikitumia chanzo kimoja cha ununuzi.

Mkaguzi Mkuu huyo anaeleza katika ripoti yake kuwa TFC ilifanya manunuzi hayo ya mabilioni bila kuzingatia kifungu cha 7 cha sheria ya manununzi ya umma ya mwaka 2013 kinachoelekeza kila taasisi ya umma kuzingatia taratibu za utoaji zabuni kama zilivyo kwenye sheria ili kuwepo thamani ya fedha.

Anaeleza kuwa manunuzi hayo yanatia shaka kwa sababu menejimenti haina nyaraka yoyote iliyoandaa kuhusu manunuzi hayo na pia hakuna kikao chochote kinachotamkwa kwenye sheria ya manunuzi ya umma kilichoketi na kuamua kufanyika kwa manunuzi hayo.

Aidha, anaeleza kuwa katika ukaguzi wake alibaini Bodi ya Zabuni iliwekwa kando kwenye mchakato mzima na kwamba TFC ilifanya manunuzi kwa kukiuka kifungu cha 159 (a) cha sheria ya manunuzi ya umma kinachoelekeza utaratibu wa kutumia chanzo kimoja cha ununuzi ufanyike kwa kuidhinishwa na Bodi ya Manunuzi.

Taarifa nyingine zinadai kuwa manunuzi hayo yalifanywa kwa maelekezo kutoka kwa kigogo mmoja wa Wizara ya Kilimo (jina lake tunalihifadhi kwa sababu hajazungumza).

Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Samuel Ahad Mshote, ameulizwa na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu kubainika kwa madudu hayo na menejimenti yake kutajwa kwenye ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani kuwa ilikiuka sheria za manunuzi ya umma, lakini hakujibu chochote.

KUJUA ZAIDI UNDANI YA MADUDU YA TFC KUHUSU MANUNUZI YA MBOLEA YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 7.9, SOMA TANZANIA PANORAMA KESHO.   

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya