Monday, December 23, 2024
spot_img

THRDC YAMPIGANIA MAKWEGA POLISI, AACHIWA, YAALANI UKIUKWAJI HAKI ZA BINADAMU

DET’U KAKELAKAMBUZI

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umewezesha kuachiwa kwa dhamana, Mwandishi wa Habari Kazimbaya Makwega aliyekuwa akishikiliwa Kituo cha Polisi Kati Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Utetezi kwa Watetezi wa Haki za Binadamu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Wakili Paul Kisabo ilieleza kuwa Makwega aliachiwa jana kwa dhamana na anatakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Kati Dodoma Machi, 2024.

Wakili Kisabo alieleza kuwa Makwega aliyekuwa akitetewa na Wakili wa THRDC, Tumaini Kakata, alikamatwa Februari 22, 2024 akiwa nyumbani kwao Malya, Jijini Mwanza na kusafirishwa hadi Kituo cha Polisi Kati cha Jijini Mwanza na siku iliyofuata alisafirishwa hadi Dodoma ambako ilisemekana tuhuma zake zimefunguliwa.

Taarifa ya Wakili Kisabo ilieleza kuwa Mkurugenzi wa Shirika la OJADACT, Edwin Soko aliomba usaidizi wa kisheria wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Bindamu THRDC kwa ajili ya kumtetea Makwega ambaye hadi anaachiwa kwa dhamana hajaambiwa tuhuma zake licha ya kuwekwa ndani kwa muda wa siku nne.

Wakili Paul Kisabo

Katika taarifa yake hiyo, Wakili Kisabo alieleza zaidi kuwa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania  unalaani kitendo cha Jeshi la Polisi kumkamata Makwega na kumuweka korokoroni kwa muda wa siku nne pasipo kumfahamisha tuhuma zinazomkabili.

“Mtandao unatoa wito kwa Jeshi la polisi kufanya upelelezi kwa kuzingatia sheria na Amri Kuu za Jeshi la Polisi (PGO). Mtandao unatoa wito kwa Jeshi la Polisi kujiepusha na utaratibu wa kuwakamata waandishi wa habari na kuwasafirisha kwenda mikoa mingine kwa madai kwamba tuhuma zao zimefunguliwa katika mikao hiyo,” inasomeka taarifa ya Wakili Kisabo.

Aidha, ilieleza zaidi kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, waandishi wa habari wana haki na uhuru wa kufanya kazi yao na hawapaswi kuingiliwa.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya