VATICAN
RAIS wa Ukreini, Volodymyr Zelenskyy amemshukuru kiongozi wa Kanisa Katoliki Duanini, Papa Francisco kwa kuunga mkono upatikanaji amani nchini kwake.
Zelenskyy alitoa shukrani hizo kwa Papa Francisco Disemba 28, 2023 alipozungumza naye kwa njia simu ambapo Papa aliitumia fursa hiyo kuwatakia wananchi wa ukreini heri na baraka katika maadhimisho ya sherehe ya Noeli kwa mwaka mpya 2024.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari za Kanisa Katoliki Daniani, Papa Francisco na Zelenskyy walijadali mpango wa amani unaopaswa kutekelezwa kwa vitendo nchini Ukreini.
Mei 13, mwaka huu, Zelenskyy alifanya ziara Vatican na kukutana na Papa Francisco na ziara yake hiyo ilitanguliwa na kikao chao cha kwanza kilichofanyika siku chache kabla ya vita baina ya Urusi na Ukreini kuanza.