Wednesday, June 18, 2025
spot_img

UTAFITI WAIWEKA TANZANIA NAFASI YA KWANZA AFRIKA KWA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

RIPOTA PANORAMA

TANZANIA imetajwa kuwa kinara wa uhuru wa vyombo vya habari barani Afrika.

Hayo yameelezwa leo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Alexander Makulilo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu hali ya siasa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwakani na uchaguzi mkuu wa 2025.

Profesa Makulilo aliwasilisha mada katika mkutano maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa uliowashirikisha wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kufanyia kazi masuala yanayohusu demokrasia.

Katika mada yake kwenye mkutano huo unaofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, Profesa Makusalo amesema utafiti kuhusu hali ya Demokrasia kwa nchi 36 za Afrika uliofanywa na Afribarometer, mwaka huu umeonyesha kuwa Tanzania ina kiwango cha juu cha uhuru wa habari.

Profesa Makusalo amesema katika utafiti huo ambao ulihusisha hojaji kwa wananchi wa nchi  husika, Tanzania ilipata asilimia 81 ikifuatiwa na Gambia ambako maoni ya wananchi wake kuhusu uhuru wa habari yalionyesha upo kwa kiwango cha asilimia 79.

Nchi nyingine ambazo utafiti umeonyesha uhuru wa habari upo kwa kiwango kikubwa ni Tunisia ambako ni asilimia 78 na Mauritania yenye asilimia 75.    

Alisema mambo mengine yaliyobainika kwenye utafiti huo yaliyoiweka Tanzania kwenye nafasi ya juu kwa ubora wa demokrasia ni kuimarika kwa uhuru wa watu kutoa maoni na kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya