Wednesday, December 25, 2024
spot_img

RAIS SAMIA: UHURU WA MAONI UNA MIPAKA

RIPOTA PANORAMA

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema uhuru wa kutoa maoni uliopo una mipaka ya kisheria na kibinadamu.

Akizungumza leo katika mkutano maalumu ya Baraza la Vyama vya Siasa na wadau wa demokrasia uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, amesema mtu aliyezaliwa, akalelewa vizuri, akasoma shule na kupitishwa kwenye masomo ya dini, yapo mambo ambayo hawezi kuyaongea.

“Kuna uhuru wa maoni lakini uhuru wa maoni una mipaka yake siyo tu kisheria hata kibinadamu. Kama ulizaliwa, ukalelewa vema, ukapitishwa kwenye masomo tunayosoma, lakini ukapitishwa kwenye masomo ya dini ukaielewa vizuri, kuna mambo huwezi kufanya tu, Kama ulipata malezi mazuri ukaijua dini yako ukakua kwenye misingi mizuri, kuna mambo huwezi kufanya,” amesema Rais Samia.

Amesisitiza kuwa uhuru wa kutoa maoni una mipaka yake kwa mtu aliyezaliwa na baba na mama yake na akalelewa vema kwa kufuata misingi ya mafundisho ya dini.

Amesema Serikali iliruhusu mikutano ya hadhara ili vyama vya siasa vipate fursa ya kuzungumza, wananachi wasikie sera na mipango yao kwa lengo la kuvikuza na kuvirudishia nguvu zao na wafuasi waliowapoteza ili ukifika wakati wa uchaguzi viwe vimejijenga vema.

Rais Samia amesema ruhusa ya mikutano ya vyama vya siasa iliyotolewa na Serikali siyo fursa kwao ya kwenda kuvunja sheria au kwenda kutukana na kuchambua dini za watu wengine; na hapo hapo amesema hashangazwi na yanayotokea kwa sababu wanaoyazungumza hawana la kuzungumza.

“Kwa hiyo tumetoa fursa hiyo na niwaombe sana vyama vya siasa tumieni hiyo fursa. Kajijengeni kwa wananchi, elezeni sera zenu, elezeni mtafanya vipi, elezeni mmejipanga vipi ili wananchi wawaunge mkono, tuikienda kwenye uchaguzi vyama vyote viwe vimesimama vizuri,” amesema.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya