Sunday, June 15, 2025
spot_img

HABARI PICHA- JAJI MUTUNGI AKUTANA NA VIONGOZI WA CHADEMA

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akiongoza mazungumzo kati ya maafisa na watendaji wa ofisi yake na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Wa kwanza kulia kwake ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe akifuatiwa na Katibu Mkuu wake, John Mnyika. Upande wa kushoto katikati ni Naibu Msajili, Sisty Nyahoza. Kikao hicho kimefanyika leo ofisi ndogo ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyopo Jijini Dar es Salaam. (Picha kwa hisani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.)

Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na maofisa wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakimsikiliza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakati wa kikao kilichofanyika leo, ofisi ndogo ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jijini Dar es Salaam. (Picha kwa hisani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.)

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, (kushoto kwake) ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa na watendaji wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika leo ofisi ndogo ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyopo Jijini Dar es Salaam. (Picha kwa hisani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.)

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akiagana na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe baada ya kumaliza kikao chao kilichofanyika ofisi ndogo ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha hiyo ni Katibu Mkuu wa Chadema, John Myika na maafisa wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. (Picha kwa hisani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.)

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akiagana na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika baada ya kumalizika kwa kikao kati yake na viongozi wa Chadema kilichofanyika leo ofisi ndogo ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyopo Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha hiyo ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na maofisa wa Ofisi wa Msajili wa Vyama vya Siasa. (Picha kwa hisani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.)

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya