Monday, December 23, 2024
spot_img

PROF. LIPUMBA AKOSA MAJIBU YA RADIO MWAMBAO, MADINI, MASHAMBA YA CHUMVI

RIPOTA PANORAMA

CHAMA cha Wanancbi (CUF), hakina taarifa zozote kuhusu uwekezaji kilioufanya katika miradi ya Radio Mwambao, maeneo ya uchimbaji madini yaliyopo mkoani Tanga na mashamba ya mkonge yaliyopo Mkoa wa Lindi.

Uwekezaji huo wa CUF katika maradi hiyo uligunduliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika ukaguzi alioufanya kwenye daftari la uwekezaji la chama hicho.

Ripoti ya ukaguzi ya CAG kwa mwaka 2021/22, inaeleza kuwa baada ya kugundua CUF kinamiliki miradi hiyo na menejimenti ya chama hicho kutakiwa kutoa taarifa kuhusu uwekezaji wake; taarifa hizo hazikupatikana.

Tanzania PANORAMA Blog imemuuliza Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuhusu mwenendo wa miradi hiyo, ikirejea hoja zilizoibuliwa na CAG na kuziombea ufafanuzi wake, lakini alishindwa kujibu chochote.

Kwa mujibu wa CAG, Menejimenti ya CUF haikutoa taarifa zozote za uwekezaji wala za mradi wakati wa ukaguzi na kwamba kukosefu kwa taarifa za miradi hiyo kulikwamisha kufahamu gharama, mapato na faida inayotokana na uwezekaji huo.

“Wakati wa ukaguzi wa daftari la uwekezaji la Chama cha Wananchi (CUF) nilibaini kuwa kinamiliki Redio Mwambao, maeneo ya uchimbani madini mkoani Tanga na mashamba ya chumvi mkoani Lindi. Hata hivyo pamoja na taarifa hizo, menejimenti ya CUF haikutoa taarifa zozote za uwekezaji wala mradi wakati wa ukaguzi.

“Ukosefu huu wa taarifa ulifanya iwe vigumu kubaini gharama, mapato na faida inayotokana na uwekezaji huo na kushindwa kutambua sehemu ya mapato ambayo CUF kinapaswa kupata ili kusaidia katika uendeshaji wa chama.

“Kwa maoni yangu, kukosekana kwa taarifa za uwekezaji kumeonyesha kuwa Bodi ya Wadhamini ya CUF, imeshindwa kufuatilia utekelezaji wa miradi hii ya uwekezaji na hivyo kuwepo hatari ya upotevu wa mapato,” anasema CAG.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya