Monday, December 23, 2024
spot_img

2023 ‘FUKO LA FEDHA’ KUKUSANYA USD BIL 85.4

RIPOTA PANORAMA

UCHUMI wa Tanzania unatarajiwa kukua hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 85.5 mwaka 2023.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba alipokuwa akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2023/24 bungeni jijini Dodoma, Juni 25, mwaka huu.

Akisoma bajeti hiyo, Dk. Nchemba alisema takwimu za Shirika la Fedha la Kimataifa (IFM) zilizotolewa Aprili, mwaka huu, zinaonyesha kuwa uchumi wa Tanzania umepanda hadi nafasi ya sita kwa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Kwa mujibu wa Jarida la Uchumi la Shirika la Fedha la Kimataifa (IFM) la Aprili 2023, uchumi wa Tanzania unatarajiwa kufikia Dola za Marekani bilioni 85.4 mwaka 2023, kutoka Dola za Marekani bilioni 69.9 mwaka 2021.

“Tanzania imepanda hadi nafasi ya sita ikilinganishwa na nchi nyingine Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiongozwa na nchi za Kenya, yenye uchumi wa Dola za Marekani bilioni 116 na Ethiopia ambayo uchumi wake ni Dola za Marekani bilioni 120.4,” alisema Dk. Nchemba.

Alizitaja nchi nyingine zenye uchumi mkubwa juu ya Tanzania kuwa ni pamoja na Angola, Dola za Marekani bilioni 121.4 Afrika ya Kusini, Dola za Marekani bilioni 405.7 na Nigeria, Dola za Marekani bilioni 477.4.

Nchi nyingine alizozitaja kuwa na uchumi mkubwa chini ya Tanzania ni Ghana ambayo ina Dola za Marekani bilioni 72.8, Ivory Cost, Dola za Marekani bilioni 70.0, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Dola za Marekani bilioni 62.8 na Uganda yenye Dola za Marekani bilioni 48.8.   

Aidha, Dk. Nchembe alisema mchakato ulioanzishwa na Serikali wa kufanyiwa tathmini ya uwezo wa kukopa na kulipa madeni, haukukamailika kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya mdororo wa uchumi pamoja na kuyumba kwa soko la fedha duniani.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya