RIPOTA PANORAMA
SURA ya Bajeti ya Serikali ya Tanzania kwa mwaka wa fedha 2023/24, inaonyesha kuwa mapato ya ndani yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) ni Shilingi trilioni 26,725,409.
Sura hiyo inaonyesha kuwa mapato yasiyokuwa ya kikodi yatakayokusanywa kutoka kwenye wizara, idara, taasisi na mamlaka za Serikali za Mitaa ni Shilingi trilioni 3,511,719, hivyo kufanya jumla ya makusanyo ya ndani ya Serikali Kuu kuwa Shilingi trilioni 30,227,128.
Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba ambaye jana alisoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24, Serikali itakapokea misaada na itakopa mikopo nafuu ya kisekta yenye jumla ya Shilingi bilioni 130,123.
Pia itapokea misaada na mikopo nafuu kwa ajili ya miradi, yenye jumla ya Shilingi trilioni 3,151,958 na misaada na mikopo nafuu (GBS) ya jumla ya Shilingi trilioni 2,184,134 ambapo jumla ya misaada na mikopo nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo itakuwa Shilingi trilioni 5,466,215 huku mapato yatokanayo na makusanyo ya halmashauri yakitarajiwa kuwa Shilingi trilioni 1,143,883.
Dk. Nchemba alisema, katika bajeti hiyo, Serikali itakopa mikopo ya kibiashara ya ndani na nje yenye jumla ya Shilingi trilioni 7,540,840 ambapo mikopo ya nje ni Shilingi trilioni 2,100,464, mikopo ya ndani ni Shilingi trilioni 1,898,316 na mikopo ya ndani (Rollover) Shilingi trilioni 3,542,061 inayofanya jumla kuu ya mapato kuwa Shilingi trilioni 44,388,067.
Kwa upande wa matumizi kutoka kwenye mfuko mkuu wa Serikali, Dk. Nchembe alisema Shilingi trilioni 2,799,374 ni kwa ajili ya malipo ya riba za ndani na Shilingi trilioni 3,542,061 kwa ajili ya malipo ya mtaji wa ndani (Rollover),
Alisema matumizi mengine katika mfuko mkuu huo wa Serikali ni ya Shilingi trilioni 2,763,947 kwa ajili ya malipo ya mtaji wa nje, Shilingi trilioni 1,364,377 kwa ajili ya kulipia riba za nje, Shilingi trilioni 1,710,608 kwa ajili ya kulipa michango ya Serikali kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na Shilingi bilioni 591,167 kwa ajili ya matumizi mengine ya mfuko, ambapo jumla yake ni shilingi trilioni 12.771,533.
Kwa mujibu wa Dk. Nchemba, Serikali itatumia Shilingi trilioni 10,882,126 kwa ajili ya kulipa mishahara, malipo ya madeni yaliyohakikiwa zitatumika Shilingi bilioni 200,000, fedha kwa ajili ya matumizi ya halmashauri (own sources) ni Shilingi bilioni 689,468 na matumizi mengineyo Shilingi trilioni 4,629,351.
Dk. Nchemba alisema fedha kwa ajili ya ruzuku ya maendeleo jumla yake ni Shilingi trilioni 1,138,369 ambapo fedha kwa ajili ya kugharamia elimu bila ada kwa shule za msingi na sekondari ni shilingi bilioni 399,642 na fedha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni Shilingi bilioni 728,727.
Dk. Nchemba alitaja jumla ya Shilingi trilioni 14,077,220 kuwa zitatumika kwa matumizi ya maendeleo; Shilingi trilioni 10,795,139 zikiwa fedha za ndani ya Shilingi trilioni 3,282,081 ni fedha za nje.
Alisema, kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 528,000 ni kwa ajili ya malipo ya madeni yaliyohakikiwa, Shilingi trilioni 1,113,000 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, Shilingi trilioni 1,500,000 zitatumika kugharamia bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, Shilingi bilioni 454,415 ni matumizi ya halmashauri na miradi mingine zitatumika Shilingi trilioni 7,199,724.
KWA WASOMAJI WETU WA TANZANIA PANORAMA BLOG; HUSUSAN WALIO NJE YA NCHI, MCHANGANUO HUU WA SURA YA BAJETI, MAPATO NA MATUMIZI, UPO KWENYE HOTUBA YA BAJETI 2023/24 ILIYOSOMWA JANA BUNGENI DODOMA NA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DK. MWIGULU NCHEMBA,. HIVYO WASIPOTOSHWE NA TAARIFA ZILIZO NJE YA HOTUBA HIYO YA BAJETI.