Tuesday, December 24, 2024
spot_img

MFUGAJI AMPIGA RISASI MKULIMA SIMANJIRO

RIPOTA PANORAMA

Simanjiro

PAUL Laizer ambaye ni mfugaji wa jamii ya kimasai, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Mkoa wa Manyara kwa tuhuma za kumshambulia kwa risasi, Walter Kaaya ambaye ni mkulima.

Taarifa kutoka eneo la tukio zimeeleza kuwa, limetokea hivi karibuni katika Kata ya Robosaiti, Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara wakati Kaaya mwenye umri wa miaka 34 akiitoa shambani kwake mifugo ya Laizer mwenye miaka 43.

Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog, dada wa majeruhi aliyejitambulisha kwa jina la Glory Kaaya amesema, mfugaji Laizer alimshambuliwa kwa risasi kaka yake Kaaya kisha akakimbilia kusikojulikana kabla ya kukamatwa na polisi akiwa amejificha kwa mganga wa kienyeji.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, George Katabazi amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kamanda Katabazi ameonya wananchi wanaomiliki silaha kuacha kuzitumia vibaya kwa kueleza kuwa matumizi mabaya ya silaha ni kuvunja sheria na pia aliwataka wananchi wanaomiliki silaha katika mkoa huo kuzingatia matumizi yake.

Glory Kaaya amesema kaka yake amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC.

“Risasi ilimpiga kifuani upande wa kulia na tunaambiwa na matabibu kuwa imeharibu huko ndani na hivi sasa mapafu yake yanatoa maji mara kwa mara kutokana na majeraha ya risasi aliyoyapata,” amesema Glory.

Walter Kaaya ambaye amejeruhiwa kwa risasi akiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC

Amesema tayari madaktari wameshamfanyia upasuaji lakini bado tatizo la kutoka maji kwenye mapafu halijaisha na kwamba kila siku madaktari wanamtoa maji kwenye mapafu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na Tanzania PANORAMA Blog, wakati mkulima huyo akitoa mifugo ya Laizer kwenye shamba lake lenye mazao mchanganyiko, Lazier alitokea vichakani ghafla na kumpiga risasi.

“Tunaomba serikali iingilie kati hii migogoro baina ya wafugaji na wakulima. Sisi wakulima tunaotesha mazao yetu lakini wenzetu wafugaji hawathamini gharama tunazotumia na badala yake wanaingiza mifugo yao kwenye mashamba yetu na kuharibu mazao yetu,” amesema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Kwa upande wake, Kamanda Katabazi amesema Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa za kutokea kwa shambulio hilo, lilianza kumtafuta mtuhumiwa aliyekuwa amekimbia na lilimkamata akiwa eneo la Nyumba ya Mungu alikokuwa amejificha.

“Wananchi walifikiri kwamba kwa kuwa mtuhumiwa ni mtu mwenye mifugo na fedha ni vigumu kukamatika, lakini sisi Jeshi la Polisi kwa weledi na maadili tulimkamata na kumtia mbaroni na sasa tunafanya utaratibu wa kumfikisha mahakamanim,” amesema Kamanda Katabazi.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya