Thursday, July 17, 2025
spot_img

MKUTANO WA UN – HABITAT WAANZA NAIROBI KENYA

RIPOTA PANORAMA

Nairobi, Kenya

MKUTANO Mkuu wa Shirika la Makazi duniani (UN – HABITAT) unaanza kesho jijini Nairobi, Kenya ukiwa na kauli mbiu isemayo hatma ya miji endelevu kupitia ushirikishwaji na uwepo wa mifumo ya mahusiano ya kimataifa.

Taarifa iliyotolewa leo jijini hapa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Simbachawene imeeleza kuwa mkutano huo ulitanguliwa na ule wa Baraza la Mawaziri duniani, wanaohusika na uendelezaji miji na makazi.

Dk. Simbachawene amesema ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo unaongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula ambaye leo aliongoza ujumbe huo kwenye Mkutano wa Baraza la Mawaziri duniani  wanaohusika na miji na makazi.

Amesema, mapema Waziri Mabula aliongoza kikao kazi cha ujumbe wa Tanzania kilichojadili namna Tanzania inavyoweza kushiriki mkutano huo kwa tija kubwa.

Balozi Simbachewene amesema katika kikao kazi hicho, Waziri Mabula aliwataka washiriki wote wa Tanzania kwenye mkutano huo kutangaza mambo mema yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya nyumba, makazi na masuala ya mazingira badala ya kuwa walalamikaji.

Kwamba, Waziri Mabula alisema ushiriki wa wajumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo utakuwa na tija kwa nchi kama watatumia fursa zitakazokuwepo kwenye mkutano huo kujifunza mambo mapya yatakayoongeza kasi ya kuendeleza nchi katika sekta ya makazi.   

Wakati huo huo, Balozi Simbachewene katika taarifa yake aliyoitoa leo kwa Waziri Mabula na ujumbe wake kuhusu maandalizi ya mkutano huo, alisema yamekamilika ipasavyo kwa Tanzania kushiriki miongoni mwa washiriki zaidi ya 3,000 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Mkutano huo utafunguliwa kesho la Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dk. William Samoe Ruto na unatarajiwa kumalizika mei 9, 2023.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya