Friday, May 30, 2025
spot_img

WIZARA YA ARDHI KUTOA HAKIMILIKI ZA KIMILA 520,000 MWAKA 2023/24

JACQUILINE MRISHO – MAELEZO

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itaandaa na kutoa Hati za Hakimiliki 520,000, Hatimiliki 500,000, Hatu za sehemu ya jengo 1,000 na kusajili miamla ya Hatimiliki na nyaraka za kisheria 100,000 kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2023/24 ya wizara hiyo bungeni Dodoma leo.

Mabula amesema wizara haikuweza kufikia malengo katika uandaaji na usajili wa Hatimiliki na Hati za Hakimiliki za Kimila kutokana na kuchelewa kuanza kwa mradi wa uboreshaji wa usalama wa milki za ardhi, kutokamilika kwa wakati miradi ya programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi (KKK) katika mamlaka za upangaji, wananchi wengi kutokamilisha ulipaji wa gharama za umilikishaji na changamoto ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Amesema hadi Mei 15, 2023, wizara imeandaa na kusajili Hatimiliki 76,746, imetoa Hati za Hakimiliki za Kimila 51,762, imeandaa vyeti vya ardhi ya kijiji 67, imesajili Hati za sehemu ya jengo 300, miamala ya hatimiliki na nyaraka za nisheria 92,124 pamoja Hatimiliki na nyaraka za kisheria 100,000.

“Kwa mwaka huu wa fedha, wizara inatarajia kufanikisha malengo hayo kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa milki za ardhi, programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi (KKK) na mradi wa kuboresha miundombinu ya upimaji na ramani kwa kushirikisha wadau wa sekta binafsi, kuimarisha mifumo ya TEHAMA ambayo itarahisisha utoaji wa Hatimiliki na kupitia upya viwango vya tozo na ada za umilikishaji ili kuleta unafuu kwa wananchi,” amesema Mabula.

Waziri Mabula amesema wizara imeendelea kuandaa na kusajili Hatimiliki na Hati za Hakimiliki za Kimila kwa wananchi na taasisi na kutoa vyeti vya kijiji ambapo umuhimu wa Hatimiliki hizo ni kuongeza usalama wa miliki na kuwezesha kupunguza migogoro ya ardhi. Vilevile, Hatimiliki hizo zinaweza kutumika kama dhamana kwenye taasisi za fedha na vyombo vya kisheria

Aidha, amewahakikishia wananchi na taasisi za fedha kuwa Hati za Hakimiliki za Kimila ni nyaraka halali za kisheria hivyo waendelee kuzitumia kwa manufaa ya kiuchumi.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya