RIPOTA PANAROMA
KAPTENI Benard Shayo, rubani wa ndege aina ya Cessina 192 yenye namba 5H-FZS amefariki dunia baada ya ndege hiyo kuanguka katika Uwanja wa Ndege ya Matambwe uliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (Nyerere National Park).
Ndege hiyo imeanguka leo, majira ya saa 5.30 asubuhi ilipokuwa ikiruka kwenye Uwanja wa Ndege wa Matambwe ikiwa na abiria watatu na rubani mmoja waliokuwa wakienda kwenye doria.
Taarifa za uhakika kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga zimeeleza kuwa watu wawili waliokuwa kwenye ndege hiyo wamefariki dunia baada tu ya kuanguka kwa ndege hiyo na wengine wawili wamejeruhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa hizo majeruhi wamepelekwa zahanati ya hifadhini kupatiwa huduma ya kwanza huku utaratibu wa kuomba ndege kwa ajili ya kuwawahisha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu zaidi ukifanyika.
Iliwataja majeruhi katika ajali hiyo ya ndege ni askari wwili, SCR Theonas Mnota na CRII Evanda Elisha na waliofariki ni Kapteni Shayo na Amani Mgogoro. Miili ya marehemu hao ilihifadhiwa kwa muda katika zahanati ya hifadhini.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Ali Changwila amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa taarifa kamili ya ajali hiyo itatolewa baadaye leo.