Monday, December 23, 2024
spot_img

HABARI PICHA, WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AKIWA BUNGENI DODOMA, MEI 5, 2023 NA ALIPOTEMBELEA MAONYESHO YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbunge wa kuteuliwa, Riziki Lulida kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Mei 5, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 2

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kata za Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera baada ya kuzungumza nao kwenye ukumbi wa Msekwa bungeni jijini Dodoma, Mei 5, 2023. WanaCCM hao walikwenda bungeni kwa mwaliko wa mbunge wao, Innocent Bilakwate. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 3

DSC Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata za Wilaya ya Kyerwa, baadhi ya wabunge na Naibu Mawaziri kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Mei 5, 2023. WanaCCM hao walikwenda bungeni kwa mwaliko wa mbunge wao, Innocent Bilakwate. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 4

Happy Kapinga akimpa maelezo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu tiba lishe, mafuta na sabuni zinazotokana na mwani katika maonyesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 2, 2023. Kulia kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 5

Happy Kapinga akimpa maelezo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu tiba lishe, mafuta na sabuni zinazotokana na mwani katika maonyesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 2, 2023. Kulia kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega na kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA NAMBA 6

DSC  1633 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi  wa Kampuni ya Alphakrust Limited, Ganeshan Vedagiri (kulia) kuhusu minofu ya samaki iliyogandishwa kwa ajili ya kuuzwa ndani na nje ya nchi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 2, 2023. kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya