Sunday, September 7, 2025
spot_img

ACT WAZALENDO ‘YAKUNJUA’ MIKONO KATIBA MPYA

RIPOTA PANORAMA

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza kupokea kwa mikono miwili agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kutaka kuitishwa kikao maalumu cha Baraza la Vyama vya Siasa kitakachotathimini utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini.

Kauli ya kupokea kwa mikono miwili agizo hilo la Rais Samia imetolewa jana na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu katika taarifa yake kwa umma iliyoeleza pia mategemeo ya chama hicho kuwa kikao kitakachoitishwa, kitakuwa sehemu ya maandalizi ya mkutano wa kitaifa wa kujadili mambo yaliyokwamisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya, mwaka 2014.

Juzi, Mei 6, Rais Samia alimuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuitisha kikao maalumu cha Baraza la Vyama vya Siasa ambacho kitawashirikisha wadau kutathimini utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.

Rais Samia alitoa agizo hilo katika kikao baina yake na viongozi mbalimbali wa Serikali kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma kikiwa na ajenda ya kuanza kwa mchakakto wa Katiba mpya.

Shaibu katika taarifa yake kwa umma ameeleza kuwa ACT Wazalendo kimekuwa kikitoa rai mara kwa mara ya kuhitaji ratiba ya utekelezaji wa mapendekezo ya kikazi kazi.

“Imekuwa ni rai ya mara kwa mara ya ACT Wazalendo kuhitaji ratiba ya utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi. Ni matumaini yetu kuwa kikao hicho kitapatiwa ratiba hiyo ambayo itahakikisha tuna sheria mpya ya uchaguzi na sheria mpya ya vyama vya siasa kabla ya mwisho wa mwaka.

“Vile vile kuhakikisha kwamba mabadiliko ya sheria ya mabadiliko la Katiba yanafanyika ili kuanza mchakato wa Katiba mpya kwa kuundwa kwa timu ya wataalamu kama ilivyopendekezwa na kikosi kazi,” inasomeka sehemu ya taarifa ya Shaibu.   

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya