Thursday, July 17, 2025
spot_img

RAIS SAMIA AMUAGIZA MSAJILI WA VYAMA KUITISHA KIKAO MAALUMU

RIPOTA PANORAMA

RAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuitisha kikao maalumu cha Baraza la Vyama vya Siasa.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Zuhura Yunus kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa Rais

Samia ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ambacho ajenda yake ilikuwa kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Samia ameelekeza lengo la kikao maalumu kitakachoitishwa na Jaji Mutungi liwe kuwashirikisha wadau kutathimini utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.

Taarifa imeeleza zaidi kuwa kikao cha leo Ikulu ya Chamwino kimejadili namna ya kuwashirikisha wadau mbalimbali na hasa ushirikishwaji wa wananchi katika mchakato huo kutoka pande zote mbili za muungano, Tanzania Bara na Zanzibar.

Imeeleza kuwa mbali na mchakato wa Katiba mpya, masuala mengine yanayotarajiwa kushughulikiwa ni marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi zikiwemo Sheria za Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro na watendaji wa taasisi mbalimbali.

HABARI PICHA RAIS SAMIA AKIWA KWENYE KIKAO NA VIONGOZI ZA SERIKALI IKULU CHAMWINO, LEO.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya