Wednesday, December 25, 2024
spot_img

JUMA RAIBU ADAIWA KUTISHIA KUWALAWITI MADIWANI WENZAKE

Diwani wa Kata ya Bomambuzi, Juma Raibu (mwenye suti nyeusi) akilishwa keki na mwanaume anayedaiwa kuwa kwenye mapenzi ya jinsia moja. Diwani Raibu alishiriki sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mwanamume huyo shoga iliyofanyikia Mgahawa wa Bondeni Lounge, Februari 13, mwaka jana

RIPOTA PANORAMA

Moshi, Kilimanjaro

DIWANI wa Kata ya Bomambuzi, Manispaa ya Moshi Mjini, Juma Raibu anadaiwa kutaka kutekeleza vitendo vya ulawiti dhidi ya madiwani wenzake.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya madiwani waliozungumzia tishio hilo zimeeleza kuwa Diwani Raibu, ambaye pia alipata kuwa Meya ya Manispaa ya Moshi Mjini kabla ya kuondolewa kwa kashfa mbalimbali ikiwemo ya kushiriki sherehe za mashoga, amekuwa akitaka kuwatendea kitendo hicho madiwani wenzake bila kificho.

Tanzania PANORAMA imeelezwa kuwa tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi kimekwishataarifiwa kuhusu hilo na kwamba taarifa ya awali kuhusu mwenendo huo wa Diwani Raibu imekwishafikishwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi.

Kwa mujibu nyaraka mbalimbali kuhusu malalamiko ya madiwani waliokumbana na kadhia ya kutaka kutendewa kitendo hicho na Diwani Raibu ambazo Tanzania PANORAMA imeziona, zinaonyesha kuwa tangu Februari mwaka jana, tishio hilo lilikuwepo.

Moja ya nyaraka ambazo Tanzania PANORAMA imeziona iliyoandikwa kwenda kwa mmoja wa viongozi wa Serikali ikiomba kuitishwa mkutano wa dharura kujadili mwenendo usiofaa wa Diwani Raibu, pamoja na mambo mengine inasomeka kuwa katika vikao vya baraza la madiwani, Diwani Raibu amekuwa akitoa lugha chafu kwa madiwani wenzake.

Kwamba Diwani Raibu amekuwa akiwaita baadhi ya madiwani wenzake ‘layman’ na ambao wamekuwa wakijaribu kuonyesha kukerwa na kauli zake anazotoa kwenye baraza, nao amekuwa akiwashambulia kuwa hawajui kitu na kwamba udiwani siyo kujua kusoma na kuandika tu.

Nyaraka hiyo inasomeka zaidi kuwa Diwani Raibu katika moja ya vikao vya baraza la madiwani, alimtaka mmoja wa madiwani wenzake anayetajwa kwenye nyaraka hiyo kwa jina la Deogratius Mallya, avue nguo ili amtendee kitendo cha aibu.

Inasomeka zaidi kuwa takwa hilo la Diwani Raibu dhidi ya Diwani Mallya lilizua mtafaruku kwenye kikao ambacho kilivurugika lakini Diwani Raibu hakuishia hapo, bali alimwambia Diwani Mallya ambaye alikuwa ameghadhabika kuwa atamtendea kitendo kama hicho mmoja wa wazazi wake.

Diwani mwingine anayetajwa kwenye nyaraka hiyo kutakiwa na Diwani Raibu kutendewa kitendo hicho ni Heavenlight Kiondo wa Kata ya Korongoni ambaye alipigiwa simu na Raibu na kuelezwa nia yake hiyo.

Alipotafutwa Raibu kwa simu yake ya kiganjani ili kujibu tuhuma anazoelekezewa, kila ilipopigwa na kuita alikata. Tanzania PANORAMA ilimtumia ujumbe kwenye simu yake ya kiganjani ikiomba kupata kauli yake kuhusu tuhuma hizo, hata hivyo nao hakuujibu.

Hata hivyo, katika mahojiano ya awali ambayo Raibu alifanya na Tanzania PANORAMA kuhusu tuhuma za kutishia kumuangamiza Diwani wa Kata ya Miembeni, Mohamedi Mushi, pamoja na kueleza kuwa Mushi anamuandama, alimshambulia kwa maneno makali ambayo Tanzania PANORAMA ilishindwa kuyatumia kwa sababu za kimaadili.

Tanzania PANORAMA imefika ofisi za CCM Wilaya ya Moshi kumtafuta Mwenyekiti, Faraji Swai na kuelezwa kuwa hayupo kwani siku zake za kufika ofisini ni Jumatatu na Alhamis tu.

Alipotafutwa kwa simu yake ya kiganjani ambayo aliipokea na Tanzania PANORAMA ikajitambulisha na kumuuliza hatua ambazo ofisi yake imechukua baada ya kufikishiwa malalamiko ya maandishi na madiwani wanaotishiwa kuingiliwa kinyume cha maumbile na Diwani Raibu, alisema hasikii vizuri kisha akataka simu ikatwe kisha apigiwe tena.

Alipopigiwa tena zaidi ya mara ya tatu, alikata simu.

Tuhuma hizi zimeibuliwa ikiwa ni miezi kadhaa imepita baada ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mjini, kumwondoa Raibu kwenye wadhfa wa umeya kwa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimuandama.

Raibu aliondolewa kwenye wadhfa wa umeya Agosti 11, mwaka jana baada ya kupigiwa kura za kutokuwa na imani naye na madiwani 20 kati ya 30 wa baraza hilo akituhumiwa kuhudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya kijana anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Raibu alihudhuria sherehe hiyo iliyofanyika kwenye Mgahawa wa Bondeni Lounge, Februari 13, mwaka jana na baadaye picha zake akiwa kwenye tikio hilo zilisambaa mitandaoni, moja ya picha hizo ilimwonyesha akilishwa keki na kijana huyo ambaye alikuwa amevaa heleni kwenye masikio yake. 

Akiwa kwenye sherehe hizo, Raibu anadaiwa kupokea ‘kilio’ cha mashoga hao na kuahidi kukipatia ufumbuzi; mashoga hao inadaiwa pamoja na mambo yao mengine, ‘walilia’ kutotambuliwa kwa haki zao za ushoga.

Mbali na hilo, Raibu pia alikuwa akituhumiwa kutumia madaraka yake vibaya, rushwa katika utoaji wa vibali vya ujenzi kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kufanyika shughuli za ujenzi wa majengo ya chini.

Katika mlolongo wa tuhuma zilizokuwa zikimuandamana ilikuwemo pia ya kutoa maamuzi ambayo hayajaidhinishwa na baraza la madiwani, kutowaheshimu wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala na kutoruhusu mjadala kuhusu vikundi vilivyoomba mikopo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya