Saturday, July 19, 2025
spot_img

KIKOSI CHA UTEKAJI, UTESAJI CHADEMA CHAANIKWA

RIPOTA PANORAMA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kina genge la kihalifu kinalolitumia kuteka, kutesa, kushambulia watu na kuwamwangia tindikali. Tanzania PANORAMA Blog imeelezwa.

Tuhuma hizi zimeanikwa na baadhi ya waliokuwa viongozi waandamizi wa Chadema ikiwa ni siku chache tu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kukaririwa na chombo kimoja cha habari akieleza kuwepo kwa vitendo vya kihalifu ndani ya chama hicho alipokuwa akizungumzia shambulio la kupigwa risasi kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hivyo, Tundu Lissu.

Akizungumza na Tanzania PANORAMA hivi karibuni kuhusu Chadema kuwa na kundi linalojihusisha na vitendo vya kihalifu, aliyekuwa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Taifa wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Ludovick Joseph alisema ni kweli kundi hilo lipo na lilihusika na matukio mengi ya utekaji, utesaji na kushambulia watu.  

“Sitakwenda kwenye details za hayo lakini ninachotaka tu kusema ni kwamba daktari yuko sahihi na actually, basically daktari mambo mengi alikuwa anafichwa.

“Hayo anayotamba kwamba anajua,….anajua machache sana ambayo amepata knowledge lakini yeye binafsi alikuwa hahusishwi kwa sababu alikuwa anafahamika yupo against, so operation nyingi yeye hakujua.

“Kwa hiyo tungesema tunakwenda kwenye details, labda tungepata mengi na ya ndani zaidi. Kwa hiyo kujibu swali lako kwa ufupi, alichosema kiko sahihi na kwamba yeye mengi hayajui bado.

“Kuhusu matukio hayo kwamba yalikuwepo ni obvious yalikuwepo na mwenyekiti alikuwa anajua. Sitaki kwenda kwenye details lakini unachoweza kunikunuu ni kwamba nimeongea na Ludovick amesema kwamba ana knowledge kwamba hayo matukio yalikuwepo na kwamba yeye mwenyewe alikuwa muhusika, walau alikuwa anajua. Hayo matukio mengi tu nayafahamu kwenye details.

“Na anasema kwamba Dk. Slaa alikuwa hahusishwi kwa sababu walikuwa wanahofia kwamba yeye anapinga, Ludovick anasema kwamba Dk. Slaa anafahamu sehemu ndogo sana ya hayo matukio anayoyazungumzia, kwa leo nafungia hapo,” alisema Ludovick.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Taifa wa Ulinzi na Usalama Taifa wa Chadwema Wuilfred Lwakatare (aliyevaa nguo za kaki) akiwa na Ludovick Joseph ambaye alikuwa msaidizi wake.

Mwingine aliyezungumzia hilo na kukiri kufahamu kuwepo kwa kundi hilo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha na pia Mhasibu wa Chadema Taifa, Samsoni Mwigamba aliyesema kundi hilo la kihalifu liliundwa mwaka 2010 na 2011.

“Tukizungumzia hayo masuala, kwanza kamanda wa anga mwenyewe, mwamba, aliwahi kuniambia wakati fulani kwamba, tukiwa tuko Karatu tunashughulika na mgogoro wa uongozi. Aliwahi kuniambia kwamba hakuna namna unaweza kushinda nchi hii na kuingia madarakani bila kuwa na jeshi lako mwenyewe.

“Kwa hiyo lazima tuimarishe red brigade ili tuhakikishe kwamba tuna mfumo wetu wa ulinzi na usalama nchi nzima. Na mimi nakumbuka miaka hiyo ya 2010, 2011 sisi tulipata ushauri wa kijana mmoja pale Arusha anaitwa (anamta jina). Huyu ni hawa watu wenye mafunzo ya ngumi na karate.

“Yeye alitufuata mimi nikiwa Mwenyekiti wa Mkoa, akamfuata katibu wangu anaitwa Amani Bulugwa, akamwambia mnajua ni kwanini polisi walipowavamia pale kwenye uwanja. Unakumbuka kule kulikuwa na tukio la watu kuandamana na kulala uwanjani wakishinikiza Lema (Godbles) apewe dhamana atoke ndani.

“Lema alikamatwa, akapelekwa mahakamani halafu mahakama ikasema dhamana iko wazi na watu wa kumdhamini wakajitokeza lakini yeye akakataa. Akasema mimi sitaki dhamana, nipelekeni huko ndani, wakampeleka ndani,” alisema Mwagamba.

Akizungumzia zaidi tukio hilo, Mwigamba alisema Lema alipopelekwa gerezani na kuanza kupata suluba za huko aliomba adhaminiwe lakini hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi yake alikataa kwa sababu yeye mwenyewe alikataa kudhaminiwa awali.

“Alipofika kule, amekaa siku kadhaa akaanza kusota, akaomba dhamana, wakaja kuomba remove order kwa hakimu aliyekuwa na kesi yake ili jamaa apewe dhamana atoke. Hakimu akawaambia dhamana ilikuwa wazi siku hiyo na wadhamini walikuwepo tayari lakini mtuhumiwa alikataa akasema yeye anataka akae ndani, msinisumbue mwacheni akae ndani. Hakimu akakataa kutoa remove order.

“Baada ya kukataa, sasa ndiyo ikabidi wa-organize maandamano mimi nikiwa Dar es Salaam makao makuu kama mhasibu wakati huo. Kwa hiyo, siku hiyo sikuwepo Arusha lakini mwenyekiti alikuwepo pamoja na Katibu Mkuu na baadhi ya viongozi wa mkoa na wilaya, wakaandaa maandamano wakaenda wakaishia pale uwanja wa NIC na wakaamua kulala uwanjani.

“Sasa usiku ule polisi wakawa wamewazingira, nafikiri ilikuwa kama alfajiri saa 10 hivi kuelekea saa 11 wakati mwamba amechoropoka amemuacha Katibu Mkuu, alimwambia nakuja sasa hivi. Majira ya saa tisa hivi alimwambia kamanda natoka nakuja sasa hivi lakini hakurudi. Saa 10 kuelekea saa 11 alfajiri polisi wakawa wamewazingira, wakawatandika vibaya sana.

“Yule kijana akamfuata katibu wangu akamwambia bwana hawa vijana wenu hawana mafunzo, hawa red brigade kwa sababu wangekuwa na mafunzo msingepigwa kama kuku namna ile. Ndiyo sisi tukamchukua tukawa tunampa hela akatufundishie sasa vijana wetu wa red brigade,” alisema Mwigamba.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samsoni Mwigamba.

Alieleza zaidi kuwa kijana huyo alikuwa akitoa mafunzo kwa red brigade nyuma ya Ofisi ya Mkoa ya Chadema na kwamba mara ya kwanza kundi hilo likiwa na mafunzo lilitumika kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

“Aliwapa mafunzo sana, mazoezi sana pale kwenye ofisi ya mkoa kwa nyuma kulikuwa kuna banda, wakawa wanafanyia mazoezi hapo. Basi tukaenda kwa mara ya kwanza tumewatumia kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, wakati ule Nassari (Joshua) akiwa anagombea uchaguzi mdogo.

“Kwa hiyo tukawa tume – organize vijana tunawalipa hela, wana mafunzo, wakawa wanazunguka jimbo zima. Wakiona tu mahali CCM wamejikusanya katika mazingira ambayo wao wanahisi kuwa wanatoa rushwa wanawavamia, wanawatandika.

“Basi baada ya kushinda ule uchaguzi, ndiyo mwenyekiti akapenda sana ule mkakati na ndiyo akaniambia hayo maneno kuwa hutuwezi kuingia madarakani bila kuwa na jeshi letu la ulinzi na usalama. Kwa hiyo lazima tuwe na watu wetu na ndiyo wakamchukua yule kijana kutoka Arusha. Akawa ndiye mratibu wa Red Brigade Taifa.

“Na alikuwa anazunguka mkoa na wilaya kwa hiyo ikawa inatengenezwa network ya red brigade Taifa, mkoa, wilaya mpaka kwenye kata. Wakachukuliwa watu wengi sana ndiyo kilichoendelea,” alisema Mwigamba.

Dk. Slaa amekaririwa hivi karibuni akieleza kuwa Chadema ilikuwa na kundi la watu waliokuwa wakijihusisha na vitendo vya kuteka na kushambulia watu na alimtaja aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Temeke kuwa mmoja wa watu waliotekwa na kushambuliwa vibaya na kundi hilo la kihalifu la Chadema kabla ya kwenda kutupwa eneo la Ununio.

Dk. Slaa ambaye alikuwa akieleza sababu za yeye kutotaka kuzungumzia shambulio la kupigwa risasi kwa Lissu kwa vile hana data kamili za tukio hilo, alisema; “Mimi sipendi kuzungumzia haya masuala ya Lissu kupigwa risasi kwa sababu sina data za kutosha. Lakini vile vile ndani ya Chadema sina uhakika kwa sababu, nikatoa cases labda ndiyo kitu ulichokitaka cha aina hiyo.

“Nikasema mimi nimeletewa taarifa ya mtu wangu aliyekamatwa, kwa maana kwamba ametekwa nyara na kwa maelezo kwamba ametekwa nyara na watu wa Usalama wa Taifa.

“Na mimi asubuhi, kesho yake, bwana huyo anaitwa Joseph, alikuwa mwenyekiti wetu wa Wilaya ya Temeke, na hiyo kesi baadaye nafikiri ilifika polisi sijui baadaye iliishia wapi.

“Huyu bwana ametekwa nyumbani kwake saa sita usiku, mimi najua ametekwa na usalama wa Taifa na nilikuwa na kesi nyingi za Usalama wa Taifa kweli kutekwa watu wangu.

“Saa sita asubuhi nikaitisha press conference, nikaisema sana Usalama wa Taifa na Serikali. Saa nane mchana huyu mtu amepatikana ametupwa maeneo ya Ununio, ameumia sana usoni.

“Lakini mwezi mmoja baadaye, kijana wangu, ofisa wa red brigade anakuja kwangu ananiambia Dk. Slaa mimi ndiye niliongoza kikosi kilichoenda kumteka nyara na tumempiga tukamtupa Ununio.

“Nikauliza kwanini mnakuja kwangu kwa sababu mimi Katibu Mkuu nilikuwa sikupewa taarifa, nikaambiwa wako viongozi wanaojua. Ukiambiwa hivyo unaendelea?

“Sasa vitu vya namna hiyo ni kweli vilikuwepo na mimi nilikuwa nimevichukia na nimesema hii siku nyingi siyo kitu kipya. Ndiyo maana lilipokuja suala la Lissu nikasema ndani ya Chadema tujitazame, tuko salama, tusinyooshe vidole kwa watu kabla sisi wenyewe hatujatizama.

“Huyo kijana ni wa kwetu, mwenyekiti wa chama wa wilaya, ametupwa na bahati nzuri nafikiri sijui upepo umepiga maana waliomtupa walisema walifikiri amekufa na wakamuacha beach na leo tunasema kuna watu wanaokotwa beach kumbe na sisi tupo. Sijui unanielewa.

“Ukiwa kiongozi, lazima uwe kiongozi wa kweli, unayesema ukweli na usimamie ukweli hata kama watu wako wamefanya vitu hivyo,” alisema Dk Slaa.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya