Saturday, July 19, 2025
spot_img

ACT WAZALENDO SINGIDA NACHO CHAMKEMEA LEMA

RIPOTA PANORAMA

CHAMA Cha ACT Wazalendo, Mkoa wa Singida kimeunga mkono kauli ya kumkemea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Godbles Lema aliyoitoa Machi Mosi, 2023.

Kimesema kinaungana na wamiliki na waendesha bodaboda nchini kukemea kauli ya Lema aliyoitoa baada ya kutua nchini akitokea uhamishoni nchini Canada aliposema bodaboda na mama lishe ni kazi ya laana.

Katika taarifa yake ya maandishi ya Machi 6, 2023 iliyotolewa na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Mkoa wa Singida kimesema katika mkutano wa hadhara alioufanya Lema baada ya kutua Arusha, hakuna jambo lolote jipya la kusisimua au lenye mvuto zaidi ya kusimulia jinsi alivyotoroka akaenda kuishi ughaibuni Canada.

“Alisema yeye mwenyewe kuwa wakati ule bodaboda ndiyo iliyomtorosha hadi akaingia Kenya, amesimulia jinsi ambavyo alipewa utaratibu wa kurejea nchini kwa salama na amani na alipewa na watu wa Serikali.

“Lema ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, ni dhahiri kuwa anajua jitihada zilizofanywa na Serikali hii kuleta suluhu katika masuala ya siasa na pia kusaidia wajasiriamali. Hakupaswa kuzungumza mambo ya uongo na yasiyo sahihi,” inasomeka taarifa hiyo.

ACT Wazalendo kinaeleza zaidi kwenye taarifa yake kuwa Sekta ya Usafirishaji inajumuisha usafiri wa anga, reli, barabara na majini na katika sekta hizo bodaboda ndiyo iliyoajiri vijana wengi na inatoa huduma wakati wote kwa wananchi wa vipato mbalimbali hususan wale wa vipato vya chini.

“Lema alipokelewa na bodaboda zinazokaribia 1000 kutoka Airport KIA na zikamsindikiza hadi Arusha Mjini, vipi leo hiyo kazi iwe ni laana?

“Alizungumza kuhusu mfumuko wa bei, anasahau kwamba hilo ni suala la dunia nzima, hata nchi zilizoendelea nazo zimekumbwa na mfumuko wa bei. Juzi huko Kenya mwanasiasa Eric Omondi na wenzake waliandamana wakishinikiza Serikali kushughulikia mfumuko wa bei.

“Lema amejisahaulisha kuwa wakati anakimbia nchi chama chake, Chadema hakikuwa na maridhiano na CCM lakini amerudi amekuta tayari kuna maridhiano yaliyosimamiwa na kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe juu ya kuimarisha demokrasia nchini chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Na hilo limewezekana kwa asilimia 79 kukiwa na michakato mingine inayoendelea hususan Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi chini ya kiongozi mzalendo Zitto Kabwe,” inasomeka zaidi.

Taarifa hiyo yenye kurasa mbili inaeleza zaidi kuwa sasa matunda ya Chadema ni kumtambua na kumualika Rais Samia katika Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

“Jana wakati Rais anazungumza na wananchi wa Arumeru mkoani Arusha aliwaambia kuwa Lema alimuaomba arudi nchini, Rais alimwambia rudi na nakufutia kesi zako zote,” linasomeka.

Taarifa hiyo inahitimishwa kwa kueleza kuwa Lema anapaswa kuwaomba radhi bodaboda na mama lishe kwa kutamka kuwa kazi zao ni za laana.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya