Friday, July 18, 2025
spot_img

RAIS SAMIA ASISITIZA SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO KWA VIONGOZI

RIPOTA IKULU

Arusha

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi kukumbushana misingi ya uongozi na taratibu za utendaji kazi serikalini kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopo.

Agizo hilo alilitoa mwishoni mwa wiki hii, mkoani Arusha alipokuwa akifungua mkutano wa faragha wa mawaziri na makatibu wakuu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa Arusha (AICC).

Rais Samia aliwataka viongozi hao kuwa na uelewa wa pamoja wa mtizamo na mwelekeo wa Serikali juu ya masuala mbalimbali na pia aliwataka kuutumia mkutano huo kukumbushana na kuelekezana namna ya kutimiza ipasavyo wajibu walionao na dhamana waliyoibeba ya kuwatumikia wananchi.

Alisema umakini na umahiri unahitajika kwa viongozi katika kutumia na kusimamia rasilimali watu, vifaa na fedha za umma pamoja na kuwa na mipango mikakati thabiti ya kutekeleza na kusimamia majukumu yao.

Rais Samia aliwataka mawaziri na makatibu wakuu hao kuyasemea mafanikio ya Serikali yaliyopatikana na kuwa wepesi kusahihisha kwa wakati upotoshaji unaofanywa dhidi ya Serikali kupitia watumishi na vitengo vya habari vilivyopo katika kila wizara.

Mkutano huo umefanyika kwa mara ya kwanza tangu Rais Samia aingie madarakani ukiwa na lengo la kuwakumbusha mawaziri na makatibu wakuu kuhusu dhana ya uongozi, sifa za kiongozi bora na utaratibu wa utoaji wa maamuzi ya kisera ndani ya Serikali.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya