Monday, December 23, 2024
spot_img

MWANAMKE ALIYEUA WANAYE WATANO ANYONGWA

BRUSSELS, UBELGIJI

Genevieve Lhermitte, Mwanamke Raia wa Ubelgiji ambaye aliwaua watoto wake watano miaka 16 iliyopita, mapema wiki hii amenyongwa hadi kufa baada ya kuomba asaidiwa kufa.

Genevieve Lhermitte alimuua mwanawe wa kiume na binti zake wanne waliokuwa na umri wa miaka mitatu hadi 14, katika Mji wa Nivelles, Februari 28, 2007 na baada ya kutekeleza mauaji hayo ya watoto wake alijaribu kujiua lakini hakufanikiwa.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 56 alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2008, kabla ya kuhamishiwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili mwaka 2019.

Kwa mujibu wa sheria za Ubelgiji, mtu anaruhusu kuchagua kuuawa ikiwa atachukuliwa kuwa na matatizo ya kisaikolojia ‘yasiyovumilika,’ na si tu mateso ya kimwili, ambayo hayawezi kuponywa.

Mtu anayechagua kuuawa lazima awe na ufahamu wa uamuzi wake huo na aweze kuelezea matakwa yake kwa njia ya busara na thabiti.

“Ni utaratibu huu maalumu ambao Lhermitte aliufuata huku maoni mbalimbali ya kimatibabu yakiwa yamezingatiwa,” alisema wakili wake.

Akizungumza na vyombo vya habari mbalimbali vya nchini Ubelgiji kuhusu uamuzi wa mwanamke huyo kuomba asaidiwe kufa, Mwanasaikolojia Emilie Maroit alisema Lhermitte aliomba anyongwe hadi kufa Februari 28, 2023 kama ishara ya kuheshimu watoto wake aliowaua.

“Huenda pia ilikuwa ni kwa ajili yake kumaliza kile alichoanza kwa sababu kimsingi alitaka kukatisha maisha yake alipowaua,” alisema mwanasaikolojia huyo.

Mauaji ya watoto hao watano yaliyofanyika mwaka 2007 na kesi iliyofuata baada ya kutekelezwa kwa mauaji hayo ilitikisa Ubelgiji na wakati wa kesi mawakili wa Lhermitte walidai kwamba alikuwa amechanganyikiwa kiakili na hapaswi kupelekwa gerezani.

Hata hivyo mahakama ilimtia hatiani kwa makosa  ya mauaji ya kukusudia na kumhukumu kifungo cha maisha jela.

Mnamo 2010 Lhermitte alifungua kesi ya kudai hadi Euro 2,655,840 kutoka kwa daktari wa akili wa zamani, akidai kutochukua hatua ndio chanzo cha kutofanikiwa kuzuia mauaji hayo, lakini aliishia kuachana na kesi hiyo baada ya miaka 10.

Mwaka 2022, watu 2,966 walikufa kupitia sheria hiyo ya kuomba kunyongwa nchini Ubelgiji ikiwa ni ongezeko la asilimia 10 la watu walioomba kunyingwa nchini humo mwaka 2021.

Ugonjwa wa Saratani unatajwa kuwa sababu ya kubwa ya watu wengi kuomba kusaidiwa  kufa na tangu mwaka 2014, Ubelgiji imeruhusu watoto kusaidiwa kufa pamoja na watu wazima ikiwa ni wagonjwa mahututi na wana maumivu makali na kwamba hatua hiyo kwa watoto ni lazima iwe na idhini ya wazazi.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya